ARSENAL YAANGUKIA PUA KWA MARTINEZ ATUA ATLETICO MADRID, MAN UTD YAMUWANIA JEROME BOATENG, CHELSEA YAONGOZA MBIO KUMNASA ALEX SONG...

Monday, 22 June 2015

ATLETICO MADRID-MARTINEZ:



Atletico Madrid imefanikiwa kumsajili mshambuliaji wa Porto Jackson Martinez kwa dau la euro milioni 35, baada ya kumkosa kwa mshambuliaji wa Juventus Carlos Tevez.

MANCHESTER UTD-BOATENG:



Louis van Gaal ana nia ya kumsajili beki wa kati wa klabu ya Bayern Munich Jerome Boateng. Manchester United wamejiandaa kutoa dau la euro milioni 28 kwa ajili ya kumpata mchezaji huyo raia wa Ujerumani.

LIVERPOOL-BACCA:



Klabu ya Sevilla imeiambia klabu ya Liverpool kwamba mchezaji wao Carlos Bacca ataigharimu klabu hiyo pauni milioni 21. Mchezaji huyo aliyefanya vema katika mshindano ya Ligi ya Europa anasakwa na kocha wa Liverpool Brendan Rodgers ila atatua Liverpool kama watafikia dau lake la uhamisho.

AC MILAN-VAN PERSIE:



AC Milan wana hamu kubwa ya kumsajili mshambuliaji mwenye jina kubwa msimu huu na inaweza kuingia kwenye mbio za kumuwania mshambuliaji wa Manchaster United Robin van Persie ambaye ameonesha nia ya kutimka klabuni hapo.

MANCHESTER UTD-LUCAS BIGLIA:



Meneja wa Manchester United Louis van Gaal ametuma maskauti katika klabu ya Lazio ili kumtazama Lucas Biglia lakini Mholanzi huyo hana nia tena na kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29.

MANCHESTER CITY-GERONIMO RULLI:



Klabu ya Manchester City wana nia ya kumsajili mlinda mlango wa Real Sociedad Geronimo Rulli, lakini watamtoa kwa mkopo katika klabu ya Valencia.

CHELSEA-ALEX SONG:



Klabu ya Chelsea imeipiku klabu ya West Ham katika mbio za kuiwania saini ya kiungo wa klabu ya Barcelona Alex Song. Mchezaji huyo ana thamani ya pauni 5 milioni.

ARSENAL-JOEL CAMPBELL:



Arsenal inatazamia kumuuza mchezaji wake Joel Campbell msimu huu na imefumgua milango kwa ofa ya pauni milioni 5, Fenerbahce na Real Sociedad ni miongoni mwa klabu zinazomuhitaji mshambuliaji huyo.

0 comments:

Post a Comment