YALIYOJIRI KWENYE ANGA LA USAJILI MAJUU...

Wednesday, 22 July 2015

ARSENAL INA MATUMAINI YA KUMNASA BENZEMA:



Azma ya Arsenal kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema imepata mwamko mpya baada ya klabu ya Real Madrid kuonesha nia yao ya kumnyakuwa mchezaji wa Borussia Dortmund Marco Reus. Arsenal wana matumaini ya kufikia dau la pauni milioni 40 kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa.

Chanzo: Daily Express
Jumanne, 7/21/2015 13:29

LIVERPOOL IMEMTOA SAKHO KWA LAZIO:



Mchezaji aliyeshindwa kung'aa katika kilabu cha Liverpool Mamadou Sakho amepewa nafasi ya kujiunga na serie A. Mchezaji huyo aliyesajiliwa kwa ada ya Pauni milioni 18 ameshindwa kuonesha makali yake katika klabu hiyo na amepewa nafasi ya kujiunga na klabu ya Lazio kwa mkopo ama kwa dili la moja kwa moja.

Chanzo: Liverpool Echo
Jumanne, 7/21/2015 13:13

MAN CITY INAONGOZA MBIO ZA KUMUWANIA OTAMENDI:



Manchester City kwa sasa wanaongoza mbio za kumnyakuwa Nicolas Otamendi mbele ya wapinzani wao Manchester United. Vilabu vyote viwili vilikutana na wawakilishi wa mchezaji huyo wikiendi na mchezaji huyo wa Kiargentina ameichagua Man City, hata hivyo watatakiwa kufikia dau la euro milioni 50.

Chanzo: Superdeporte
Jumanne, 7/21/2015 14:17

INTER MILAN WAMKATAA BALOTELLI:



Liverpool wanajitahidi kumuondoa Mario Balotelli katika kilabu hicho, huku Inter Milan wakimkataa mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia. Balotelli alipambana katika msimu wake wa kwanza kilabuni hapo na kwa sasa anapatikana kwa ajili ya uhamisho.

Chanzo: Daily Express
Jumanne, 7/21/2015 13:45

ASTON VILLA YAJIUNGA KWENYE MAWINDO YA DESTRO:



Aston Villa wamejiunga kwenye kinyang'anyiro cha mshambuliaji wa kilabu cha Roma Mattia Destro. West Ham walijitokeza kama waongozaji wa mbio hizo za kuiwania saini ya raia huyo wa Italia lakini Villa, wanaotazamiwa kuwa na fedha taslimu kama Liverpool watakamilisha usajili wa Benteke, watatoa upinzani kwa West Ham.

Chanzo: Daily Express
Jumanne, 7/21/2015 13:41

CRYSTAL PALACE-ALEXANDRE PATO:



Crystal palace wamepewa mwanya wa kumsajili mshambuliaji wa Kibrazili Alexandre Pato. Mchezaji huyo wa zamani wa AC Milan amekuwa akijaribu kuuzwa kwa vilabu vya Ligi Kuu Uingereza na inasemekana kuwa yupo tayari kutua Ligi Kuu. West Ham wameonesha nia ya kumsajili pia.

Chanzo: Daily Maily
Jumanne, 7/21/2015 13:35

SUNDERLAND YAMUWANIA DEMBELE:



Sunderland inatazamia kuivamia tena Tottenham kwa mara nyingine katika harakati za kumuwania kiungo wake Mousa Dembele.

Chanzo: Metro
Jumanne, 7/21/2015 15:45

LUIS ANAKARIBIA KURUDI ATLETICO:



Atletico Madrid wanakaribia kukamilisha makubaliano ya kumchukua beki wa kushoto wa klabu ya Chelsea Filipe Luis kwa mkopo.

Chanzo: Gianluca di Marzio
Jumatatu, 7/20/2015 18:27

INTER INAMNYEMELEA DROGBA:



Inter ina nia ya kumsajili Didier Drogba. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 37 tayari amekwisha fanya mazungumzo juu ya hatua ya kuhamia MLS.

Chanzo: Daily Mirror
Jumatatu, 7/20/2015 17:15

WEST BROM-LAMBERT:



West Brom wapo tayari kutoa dau la pauni milioni 3 ili kumpata mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Rickie Lambert.

Chanzo: Daily Telegraph
Jumatatu, 7/20/2015 17:11

0 comments:

Post a Comment