BAADA YA KUMKOSA RADJA, SKRTEL NJE, KOVACIC NDANI LIVERPOOL

Wednesday, 10 June 2015

Liverpool inaonekana kumkosa kiungo Radja Nainggolan.

Kiungo huyo ambaye anamilikiwa na mawakala wawili anaripotiwa kufanya mazungumzo na klabu ya Roma ili kujiunga nao moja kwa moja.

Nainggolan amekuwa pia kivutio kwa klabu ya Manchester United lakini ripoti kutoka Italia zinasema mchezaji huyo mwenye umri wa miak 27 atabaki na klabu ya Roma.




Liverpool imejiandaa kumtoa beki wao Martin Skrtel ili kupata saini ya nyota wa Milan Mateo Kovacic.

Kwa mujibu wa habari kutoka Italia, Milan hawana nia ya kumuuza mchezaji huyo raia wa Croatia kwa dau lolote chini ya £18m isipokuwa kama Martin Skrtel atakuwa sehemu ya mabadilishano.



Lakini, kutokana na Skrtel kuonekana kutokuwa na furaha katika klabu yake ya sasa baada ya kukataa kusaini mkataba mpya, huenda akatimkia katika klabu hiyo ya Milan.

Akizungumza na Slovakian publication Aktualne, Skrtel alisema:"Kwangu haikubaliki. Nadhani kwamba aina ya mkataba uliotolewa huwa unatolewa kwa wachezaji wenye umri mkubwa zaidi yangu au wachezaji wenye matatizo ya kiafya."



0 comments:

Post a Comment