BAADA YA VERMAELEN KUJIUNGA BARCELONA, REAL MADRID WAGONGA HODI ARSENAL...

Thursday, 25 June 2015



Klabu ya Real Madrid imesema kwamba kama beki wake wa kati Sergio Ramos atatimka klabuni hapo basi itafanya juu chini kumpata mlinzi wa kati wa klabu ya Arsenal Laurent Koscielny kwa ada ya pauni milioni 21.5.

Kwa mujibu wa France Football, Laurent Koscielny aliongeza mkataba mpya na klabu ya Arsenal msimu uliopita, ametakiwa na kocha wa klabu ya Real Madrid Rafa Benitez kama mchezaji ambaye ataimarisha safu ya ulinzi wa kikosi chake baada ya Sergio Ramos kuondoka klabuni hapo.

Inaaminika kwamba mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania ameomba kutimka klabuni hapo na kujiunga na Manchester United baada ya matakwa yake kushindwa kufikiwa.



Pepe na Raphael Varane wamehusishwa pia katika tetesi za kutimka klabuni hapo, huku klabu ya Chelsea ikimfuatilia Varane kwa ukaribu zaidi.

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger yupo katika wakati mgumu kwa sasa wa kuwabakiza wachezaji nyota katika kikosi chake kwa ajili ya kuwania mataji msimu ujao.

0 comments:

Post a Comment