Dylan Kerr wa Simba, Donald Ngoma na James Zutah wa Yanga wawasili nchini...

Sunday, 28 June 2015

Dylan Kerr wa Simba, Donald Ngoma na James Zutah wa Yanga wawasili nchini tayari kwa kumaliza taratibu nakuanza vibarua vyao vipya

Donald Ngoma na James Zutah wa Yanga wawasili nchini
Dylan Kerr wa Simba, Donald Ngoma na James Zutah wa Yanga wawasili nchini

WACHEZAJI wapya wa Yanga, Donald Ngoma na kiungo raia wa Ghana James Zutah wamewasili nchini Jumamosi kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kujiunga na mabingwa hao wa msimu uliopita.

Katibu wa Yanga Dk Jonas Tiboroha ameiambia Goal kuwa zoezi la kwanza litakuwa ni kuwapima afya zao, kisha masuala ya kumalizana nao kimkataba yatafuatia wakati wowote.

Wamekuja kwa ndege ya KQ kwa wakati mmoja na kupokelewa na katibu Dk Tiboroha, katabaro na Ndama.

Kiungo James amekuja kuchukua nafasi ya Lansana Kamara aliyeshindwa kumridhisha kocha Hans van der Pluijm.


Dylan Kerr wa Simba awasili nchini

Kocha Mkuu mpya wa Klabu ya Simba, Muingereza Dylan Kerr amewasili nchini Jumamosi akiwa sambamba na kocha wa makipa raia wa Kenya Abdul Iddi Salim.

Kerr ameiambia Goal amekuja nchini kuanza kazi na anamatumaini makubwa atafanya viuri kutokana na kulijua vyema soka la Afrika.

Amesema anajua Simba ni timu kumbwa Tanzania na atajitahidi kutoa kila alichokuwa nacho ili kuipa mafanikio timu hiyo iliyomaliza nafai ya tatu msimu uliopita.

Kerr ametua nchini kuchukua nafasi ya Goran Kopunovic aliyeshindwa na uongozi wa Simba kuhusu maslahi yake ya kuongeza mkataba mpya.

0 comments:

Post a Comment