FALCAO ATUA CHELSEA, MAN CITY YAMTAKA DI MARIA ETIHAD, MADRID KUMUUZA CASILLAS SPURS....

Sunday, 14 June 2015

CHELSEA:


Mshambuliaji wa Monaco na timu ya taifa ya Colombia Radamel Falcao amejiunga na mabigwa wa ligi kuu Uingereza Chelsea baada ya kukubaliana na miamba hao kuhusu masharti ya mkataba siku ya Jumamosi.

MANCHESTER CITY:


klabu ya Manchester City iliyoshikilia nafasi ya pili ligi kuu Uingereza msimu ulioisha 2014/2015, in nia ya kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Real Madrid Angel Di Maria anayekipiga Manchester United. Txiki Begiristain amewaomba wawakilishi wa mchezaji huyo kuzungumza nae kama atakuwa tayari kujiunga na Man City kutoka Man Utd.

ARSENAL:


Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ameamua kuelekeza nguvu zake kwa kiungo wa Bayer Leverkusen Lars Bender mwenye thamani ya pauni milioni 18.

MANCHESTER UNITED:


Mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza na klabu ya Manchester United Wayne Rooney amemsihi kocha wake Louis van Gaal kumleta mshambuliaji mwenzake wa timu ya taifa na klabu ya Tottenham Harry Kane. Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Uingereza anaamini kuwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21 atafanikiwa zaidi kama akijiunga na klabu hiyo yenye makazi yake mjini Manchester. Harry Kane anasadikika kuwa na thamani ya pauni milioni 40.

LIVERPOOL:


Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers anaongoza katika mbio za kuwania saini ya mshambuliaji wa klabu ya QPR Charlie Austin. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anasakwa pia na klabu ya Newcastle United.

REAL MADRID:


Klabu ya Real Madrid ipo tayari kumuuza Iker Casillas ambaye anaweza kujiunga na mahasimu wa Arsenal klabu ya Tottenham. Kipa wa Tottenham Hugo Lloris anatazamiwa kuwa mbadala wa kudumu wa golikipa wa Manchester United David De Gea.

0 comments:

Post a Comment