FIRMINO ASAJILIWA LIVERPOOL RASMI...

Wednesday, 24 June 2015

Official: Liverpool sign Roberto Firmino

Klabu ya Liverpool imekamilisha usajili wa mchezaji wa Hoffenheim Roberto Firmino kwa ada isiyofahamika, huku akitegemea kufanyiwa vipimo vya afya.

Mkurugenzi wa Liverpool Ian Ayre alielekea Chile kwa ndege, ambako Firmino anashiriki mashindano ya Copa America ili kumalizia usajili huo unaosadikika kuwa umegharimu euro milioni 40.

Baada ya mashindano hayo kumalizika, mchezaji huyo atafanyiwa vipimo vya afya.



Klabu nyingine zilizokuwa zikimuwania mchezaji huyo ni pamoja na Manchester United.

0 comments:

Post a Comment