GIROUD ATIA AIBU MECHI YA KIRAFIKI DHIDI YA ALBANIA...

Sunday, 14 June 2015



Mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Ufaransa na timu ya taifa ya Albania imeleta hali tofauti baada ya timu hiyo ya Albania inayoshikilia nafasi ya 51 katika viwango vya ubora duniani kuichapa timu ya taifa ya Ufaransa inayoshikilia nafasi ya tisa, mchezo ulioshuhudiwa Albania ikiibuka kinara kwa ushindi wa bao 1-0.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya Arsenal Oliver Giroud, aliyepewa nafasi katika mechi hiyo baada ya mchezaji wa Real Madrid Karim Benzema kupumzishwa, hakuwa na msaada wowote jioni hiyo na alitolewa mapema baada ya kipindi cha kwanza cha mchezo huo.

Bila shaka, hakuna hitimisho lolote linaloweza kufikiwa baada ya Giroud kuonekana kutokuwa na mchango katika mechi hiyo ya kirafiki, ambapo mshambuliaji huyo alifanikiwa kupiga pasi tisa tu na kugusa mpira mara 13 ikisemekana kuwa ni kiwango chini zaidi kulingana na mipira aliyogusa kipa Hugo Lloris.

0 comments:

Post a Comment