HABARI NJEMA KWA MASHABIKI WA ARSENAL...

Thursday, 18 June 2015



Santi Cazorla ameondoa hofu iliyokuwa imetanda kwa mashabiki wa Arsenal kuhusiana na mchezaji huyo kutimka klabuni hapo kujiunga na klabu ya Hispania Atletico Madrid lakini  Santi amesema hawezi kutimka Arsenal. Cazorla amesema ana furaha Arsenal na wala hana mpango wa kuondoka.

"Tetesi kuhusiana na Atletico Madrid ni za uongo. Kwasasa, mawazo yangu yapo Arsenal. Nina miaka wiwili iliyobakia kwenye mkataba wangu na nina imani nitaimaliza," kiungo huyo aliimbia Goal.

"Nina furaha sana Arsenal na Ligi hii pia. Nahisi kupendwa na kuthaminiwa na timu pamoja mashabiki."

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 alikuwa ni chaguo la Arsene Wenger katika nafasi ya kiungo msimu uliopita na pia kama mchezaji wa msimu wa klabu hiyo.

"Sifahamu kama msimu huu ulikuwa bora sana katika maisha yangu ya soka lakini nimejisikia vizuri kuwa na timu hii, kucheza katika nafasi mpya ambayo huwa najisikia vizuri nikicheza," Cazorla aliongezea. "Nina tumai nitakuwa bora zaidi msimu ujao.

"Kama tunahitaji kuchukuwa ubingwa wa ligi, ni lazima kudumisha kiwango kama tulivyokuwa katika mzunguko wa pili wa msimu uliopita. Nadhani kuwa tunahitaji kapigana na klabu za Chelsea, Manchester Utd, na Manchester City, watakuwa imara zaidi msimu ujao.

"Tunafuraha kushinda kombe la FA tena, ni muhimu sana kwa sisi kushinda mataji na sasa tunajiandaa vema na msimu ujao. Tunataka kufika hatua ya juu zaidi katika ubora wetu na nina matumaini tutapigania Ligi Kuu na kwenda zaidi katika Ligi ya Mabingwa."

0 comments:

Post a Comment