GOLIKIPA wa Tottenham Hotspur, Hugo Lloris amekiri anataka kuondoka ndani ya timu hiyo kwenda kucheza katika timu inayoshiriki Ligi ya Mabingwa. Lloris kwa sasa anadaiwa kutakiwa kwa udi na uvumba na Manchester United ambayo inamtaka golikipa huyo kurithi mikoba ya David de Gea. Lloris, 28, toka aondoke Lyon na kutua Spurs miaka mitatu iliyopita amejikuta akishindwa kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya kutokana na timu yake kutofuzu. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa alikuwa akicheza Ligi ya Mabingwa akiwa na Lyon, lakini ndani ya Spurs mambo ni magumu. Mlinda mlango huyu ni chaguo la Manchester United, ambayo inafahamu fika David de Gea anaondoka katika kikosi hicho.









0 comments:
Post a Comment