"HUMPENDI MESSI?, HUJUI LOLOTE KUHUSU MPIRA"-TEVEZ

Saturday, 13 June 2015



Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina Carlos Tevez amesema kwamba mtu yeyote asiyemkubali mchezaji mwenzake Lionel Messi hajui lolote kuhusu mpira.

Leo saa sita usiku timu ya taifa Argentina itamenyana vikali dhidi ya timu ya taifa ya Paraguay katika mashindano ya Copa America kundi B, na Messi akitegemewa kuwa mchezaji kivutio katika michuano hiyo huku mchezaji mwanzake Tevez akitegemea kuanzia benchi katika mchezo huo.

Mshambliaji huyo wa Barcelona na mshindi wa tuzo za Ballon d'Or mara nne, alikiongoza kikosi hicho cha Argentina katika mashindano ya kombe la dunia na kufikia hatua ya fainali huku mchezaji mwenzake Tevez akiachwa na aliyekuwa kocha wa timu hiyo Alejandro Sabella.

Hata hivyo, Carlos Tevez anabakia kuwa mchezaji maarufu zaidi ya Lionel Messi  nchini kwao Argentina huku akisifika zaidi kama "Mchezaji wa Watu."



Lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 anasema Messi anahitaji kupewa heshima ya kipekee kutoka kwa mashabiki wa taifa hilo.

"Naamini watu wanampenda Messi kwasababu ni Muargentina na ni bora zaidi duniani," Tevez aliiambia tovuti rasmi ya Copa Amerika katika mahujiano.

"Yeyote asiyempenda Messi hajui chochote kuhusu mpira na sijui ni nini anawaza katika kichwa chake," aliongezea.



Tevez anajichukulia kama mchezaji mzuri tangu kushuka kwa kiwango chake miaka ya karibuni na anaamini Messi ana nufaika kwa kupungua uzito hivi karibuni.

"Nina upungufu wa kilo 8," alisema. "Ninafikiri nipo vizuri kiumbo, kihisia na kimchezo. Nipo bora zaidi ya nilivyokuwa zamani."

"Messi hajabadilika. Ila kilichobadilika ni kwamba amepunguza kilo tatu au nne tofauti na zamani. Hii inamaanisha ana ari zaidi, inabadilisha akili yako, inabadilisha kila kitu."

"Naamini huu ni wakati wake kwa sasa."

0 comments:

Post a Comment