
Mkongwe wa Brazili Ronadinho Gaucho anaamini kuwa klabu ya Liverpool imepata suluhisho la ukame wa magoli klabuni hapo.
Bosi wa Liverpool Brendan Rogders anaamini kuwa mchanganyiko wa Samba ya Coutinho na Firmino ambaye amesajiliwa hivi karibuni utaongeza msisimko katika uwanja wa Anfield msimu ujao.
Huku klabu ikiendelea kumfukuzia mshambuliaji wa Sevilla Carlos Bacca- na huku wakimngojea mshambuliaji wao Daniel Sturridge ambaye yupo nje kwa majeruhi, Ronadinho anaamini ya kuwa klabu ya Liverpool haitakuwa na la kujitetea kama hawataimarika kutokana na kuwa na magoli machache msimu uliopita.

Mshindi huyo wa kombe la dunia mwaka 2002 alisema, "Ni mafanikio makubwa kwa Liverpool kuwapata Coutinho na Firmino. Itawapa moja kati ya viungo matata barani Ulaya. Ubunifu, akili na malengo waliyonayo kati yao itaibadilisha Liverpool kama timu kwa ujumla. Kuwa na viungo kama hao wawili kunawapa nafasi kubwa ya kufuzu katika Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
"Ni ndoto kwa washambuliaji wa Liverpool kuwa na huduma kama hiyo. Kama huwezi kufunga magoli katika timu ukiwa na viungo kama Coutinho na Firmino, huwezi kufunga katika timu nyingine yoyote. Watatengeneza nafasi nyingi."

Firmino mwenye umri wa miaka 23 ni habari nyingine katika soka, ametundika magoli 49 katika mechi 153 akiwa katika klabu ya Hoffenheim. Mchezaji huyo mwenye thamani ya euro milioni 28 ameisaidia nchi yake kufikia hatua ya robo fainali, akifunga goli dhidi ya Venezuela.
Anauwezo wa kucheza nafasi tofauti tofauti uwanjani. Ingawa alianza michuano akiwa na Hoffenheim kama kiungo wa kati mshambuliaji, Firmino anaweza kucheza nafasi zote za pembeni na pia kama mshambuliaji wa kati-akiwa ameshaifanyia hivyo nchi yake.
Firmino atua Liverpool
Klabu ya Liverpool imekamilisha usajili wa mchezaji wa Hoffenheim Roberto Firmino kwa ada isiyofahamika, huku akitegemea kufanyiwa vipimo vya afya. Mkurugenzi wa Liverpool Ian Ayre alielekea Chile kwa ndege, ambako Firmino anashiriki mashindano ya Copa America ili kumalizia usajili huo unaosadikika kuwa umegharimu euro milioni 40. Baada ya mashindano hayo kumalizika, mchezaji huyo atafanyiwa vipimo vya afya.
Jara aoneshwa mlango wa kutokea baada ya kuchafua hewa
Baada ya kumfanyia mambo machafu mchezaji wa Uruguay Edinson Cavani, mchezaji wa klabu ya Mainz Gonzalo Jara ameambiwa na klabu yake kuwa haitovumilia kitendo hicho na anaweza kutimka klabuni hapo mara tu ofa yoyote itakapopatikana.
Real Madrid yakataa ofa ya Man Utd
Real Madrid wametaa dau la kwanza lililotolewa na klabu ya Manchester Utd kwa ajili ya kumpata beki wa kati wa klabu hiyo Sergio Ramos. Miamba hiyo ya Hispania imepanga kumuuza beki huyo kwa dau la pauni milioni 64 na haitahusisha usajili wa kipa David De Gea kama klabu ya Manchester Utd ilivyokuwa ikihitaji.
Pogba kutua Man City kabla ya Sterling
Manchester City wanataraji kukamilisha usajili wa kiungo mfaransa Paul Pogba. Usajili huo unatazamiwa kukamilika hata kabla ya usajili wa winga wa Liverpool Raheem Sterling.
Cech ndani, Ospina nje Arsenal
Klabu ya Arsenal inaweza kumuuza golikipa wake David Ospina licha ya kufanya vema mzunguko wa pili wa msimu uliopita. Klabu ya Fenerbahce imeonesha nia kubwa ya kumuwania kipa huyo huku kipa aliyeonekana kusuasua mara kwa mara Wojciech Szczesny akitegemewa kuwa msaidizi wa Petr Cech.
"KUWA NA MCHEZAJI KAMA FIRMINO NI SAWA NA KUWA NA LULU MKONONI"-RONADINHO GAUCHO.
Popular Posts
-
Mchezaji wa zamani wa klabu ya Real Madrid Ramon Calderon anafikiria kuwa klabu ya Manchester United itakuwa imetumia hekima kumsajili Ser...
-
ARSENAL INA MATUMAINI YA KUMNASA BENZEMA: Azma ya Arsenal kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema imepata mwamko mpya baada ...
-
KIIZA APEWA WIKI MBILI KUONGEZA KIWANGO
-
Chile imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Copa America baada ya kuichapa Uruguay 1-0, lakini mapema kipindi cha pili mshambuliaji...








0 comments:
Post a Comment