LeBRON JAMES KUMVUA TAJI LA UFALME MICHAEL JORDAN...

Wednesday, 17 June 2015

LeBron James

Fainali za NBA ni wakati ambapo wachezaji wanaweza kuandika majina yao katika vitabu vya historia vya mchezo wa kikapu. Ni fursa ya kuinuka na kukumbukwa daima. Kwa LeBron James , ina maana ya kuchukua ufa mwingine katika kuchukua hatua moja karibu na kumvua taji Michael Jordan kama mchezaji mkubwa katka historia ya NBA. Ili James kushinda, anapaswa kuendelea kuonesha utendaji wa kipekee. Kuona namna utendaji wake katika Game 5 unamuweka katika safu ya juu za wakati wote.


5. Bill Russell-1962

Boston Celtics

Pamoja na michezo 7 ya mwaka 1962 ya fainali za NBA, Boston "The Celtics" walihitaji mtu wa kuongeza kiwango chake cha uchezaji ili kuibuka washindi katika muda wa nyongeza. Hakuwa mtu mwingine zaidi ya Bill Russell, ambaye aliweka kumbukumbu ya pointi 30 na ribaundi 40 kuipatia Boston ushindi wao wa nne kati ya michuano nane mfululizo.

4. Isiah Thomas-1988

Isiah Thomas

Mchukie au mpende, hakika Isiah Thomas alikuwa ni mchezaji mwenye kipaji. Alithibitisha hilo tu kwenye Game 6 za fainali za NBA mwaka 1988. Mpaka sasa, haijafahamika ni namna gani aliweza kuendelea kucheza baada ya kupata majeraha makubwa ya kifundo cha mguu. Hata hivyo, alifanikiwa kwa kufunga pointi 43, ikijumuishwa na pointi 25 alizozipata kwenye fainali za NBA. Pistons walipoteza mchezo huo, lakini juhudi za Thomas zitaishi daima.

3. Magic Johnson -1980

Magic Johnson

Pasipokuwa na msaada kutoka kwa Kareem Abdul-Jabbar, Magic Johnson alitambua kwamba anahitaji kuongeza juhudi zake binafsi ili kuiongoza Lakers kupata ushindi katika Game 6 dhidi ya 76ers. Johnson alianzia kati na kuweka rekodi ya kuvutia ya wakati wote. Pointi zake 42, ribaundi 15 na pasi za magoli 7 vilitosha sana kuipatia Los Angeles taji la NBA.

2. Michael Jordan-1997

Michael Jordan

Jordan aliweka rekodi ya pointi 38, ribaundi 7 na pasi za magoli 5 wakati akipambana na mafua. Kukaukiwa maji na uchovu ni sababu mbili zilizotaka kumuweka nje ya Game 5 dhidi ya Jazz. Pasipo kukaa nje na kupotezea mchezo huo, alijilazimisha mwenyewe na kufanikiwa kuipatia ushindi Bulls. Matokeo yalikuwa yanawapatia Chicago faida ya 3-2, ambayo yangeongezea ushindi wao wa tano katika miaka sita.

1. LeBron James-2015

LeBron

James ameweka pointi 47, ribaundi 14 na pasi za magoli 11 na kumpatia triple-double mara tatu kwenye fainali za NBA. Kwa kuzingatia kuna triple-double tano tu katika historia, inashangaza kushuhudia alichokifanya.
Kwa namna fulani, juhudi za James hazikuweza kutosha kushinda mchezo dhidi ya Warriors, lakini hiyo haichukui thamani ya yeye kuwa mchezaji bora wa wakati wote. 

0 comments:

Post a Comment