MANCHESTER UNITED YATOA €40M KWA RAMOS,FAOUZI GHOULAM KUTUA ARSENAL,OFA YA CHELSEA YAKATALIWA,POGBA AWEKEWA OFA TATU........

Tuesday, 30 June 2015

MANCHESTER UNITED - SERGIO RAMOS

Manchester United wemeripotiwa kutenga dau la euro milioni 40(€40m)  katika jitihada za kumsajili beki wa Real madrid Sergio Ramos.

ARSENAL - FAOUZI GHOULAM

Arsenal wanajiandaaa kuipatia Napoli £9m kwa ajili ya Faouzi Ghoulam wiki hii. Beki huyo wa kushoto mwenye umri wa miaka 24 pia amekuwa akiwaniwa na klabu ya Chelsea na Manchester City, lakini Arsenal wamevutiwa na mchezaji huyo na kuanza kuitafuta saini yake.

CHELSEA - ASMIR BEGOVIC & JOHN STONES

Ofa ya Chelsea ya pound milioni 6(£6m) imekataliwa na klabu ya Stoke City kwa ajili ya kumsajili golikipa Asmir Begovic ambaye anatarajiwa kuwa mrithi wa Petr Cech. Potters wanahitaji pound milioni 10(£10m) kwa ajili ya golikipa huyo mwenye umri wa miaka 28.


Chelsea wanajiandaa kumsajili beki wa Everton John Stones. Kijana huyo wa Toffees kwa sasa thamani yake inasadikiwa kuwa £20m.

BARCELONA,CHELSEA,MANCHESTER CITY - PAUL POGBA

Juventus imepokea Ofa tatu kutoka Barcelona waliokuwa wametoa €80m pamoja na €10m kama nyongeza kutokana na thamani ya Paul Pogba, ambaye anatarajia kujiunga na mabingwa hao wa UEFA msimu ujao. Chelsea wakaweka €50m pamoja na Oscar kwa matumaini ya kumpata mchezaji huyo haraka iwezekanavyo, pia Manchester City wakaweka ofa ya  € 100m kwa ajili ya kiungo huyo.


0 comments:

Post a Comment