MESSI KUFIKISHWA MAHAKAMANI...

Thursday, 11 June 2015


SIKU chache baada ya kutwaa taji la Uefa Champions League, zimetoka taarifa mbaya kwa mashabiki wa  mshambuliaji wa Barcelona na Argentina, Lionel Messi kwamba atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kukwepa kulipa kodi, baada ya mahakama ya juu ya Hispania kutupilia mbali rufaa yake.
Messi na baba yake, Jorge, wanatuhumiwa kutolipa kodi ya Euro milioni 4.1 sawa na Paundi milioni 3 katika miaka ya 2007, 2008 na 2009.
Mahakama kuu ilisema Messi asipewe dhamana kwa kisingizio cha kutofahamu utaratibu wa masuala ya fedha zake pamoja na kodi.

0 comments:

Post a Comment