PODOLSKI AITWA EVERTON, NEYMAR AJIFUNGA BARCELONA......

Monday, 15 June 2015



Meneja wa klabu ya Everton Roberto Martinez amesema ana nia ya kumleta klabuni hapo mshambuliaji wa kimataifa wa Ujerumani na klabu ya Arsenal Lukas Podolski ambaye anaonekana kutokuwa na namba kwa washika bunduki hao wa Uingereza. Mshambuliaji huyo ameaambiwa anaweza kuondoka klabuni hapo kuichezea klabu nyingine msimu ujao, na klabu ya Everton ipo tayari kumchukua mshambuliaji huyo.




Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil na klabu ya Barcelona Neymar Jr, ameongeza mkataba na miamba hao ambao utamuweka klabuni hapo hadi mwaka 2020, na atalipwa Euro milioni 12 kwa msimu.

0 comments:

Post a Comment