MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga TP Mazembe Mbwana Samatta, amesema kwa sasa hana mpango wa kucheza Ligi ya Vodacom Tanzania bara hadi ipite miaka 20 ijayo kutokana na malengo aliyokuwa nayo.
Samatta ameiambia Goal, malengo yake kwa sasa ni kucheza soka barani Ulaya ili kuzidi kupandisha kiwango chake na siyo ligi ya Vodacom ambayo bado ipo nyuma kiushindani.
“Ndoto zangu kwa sasa ni kucheza soka barani Ulaya kwenye klabu kubwa duniani na siwezi kurudi kucheza nyumbani Tanzania kwa sababu bado lengo langu halija timia,”amesema Samatta.
Samatta alijiunga na TP Mazembe mwaka 2011 akitokea klabu ya Simba baadhi ya timu za Tanzania ikiwepo Azam zilitaka kumrudisha nchini azichezee lakini aligoma kutokana na kutotimiza malengo yake aliyojipangia.









0 comments:
Post a Comment