ATLETICO MADRID YAMRUDIA SANTI CAZORLA, MAN CITY YATOA EURO MILIONI 100 KUMNASA POGBA...

Friday, 3 July 2015

ATLETICO MADRID-SANTI CAZORLA:



Klabu ya Atletico Madrid inamuwania kiungo wa klabu ya Arsenal Santi Cazorla kama mbadala wa Arda Turan ambaye anatazamiwa kutimka klabuni hapo. Mabingwa wa Ligi ya Mabingwa klabu ya Barcelona ndio inaonekana kuwa kimbilio la kiungo huyo wa Atletico na klabu hiyo imejiandaa kutoa kitita cha euro milioni 35 (pauni milioni 24.8). Kama klabu hiyo itamkosa Cazorla basi kocha wa klabu hiyo Diego Simeone amesema kuwa atamtwaa mchezaji wa Roma Miralem Pjanic. Roma wanataka euro milioni 45 kwa yeyote anayemuwania mchezaji huyo.

MAN CITY-PAUL POGBA:



Manchester City inaongoza mbio za kuiwania saini ya kiungo wa Juventus Paul Pogba. Klabu hiyo imeandaa dau la euro milioni 100 sawa na pauni milioni 71 kwa ajili ya kumrudisha kiungo huyo mjini Manchester.

0 comments:

Post a Comment