FALCAO AELEKEA CHELSEA RASMI,TURAN AITOSA MANCHESTER UNITED,EVERTON YAMPATA MBADALA WA COLEMAN,MANCHESTER CITY WARUDI KWA KEVIN.....

Wednesday, 1 July 2015

CHELSEA - FALCAO

Radamel Falcao amekubali kujiunga kwa mkopo na klabu ya Chelsea na uhamisho wa mchezaji huyo kutoka Monaco umepangwa kukamilika wiki ijayo. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Colombia aliambiwa ahudhurie kwenye mazoezi na Blues kwa ajili ya kujianda na msimu ujao.

UNITED - ARDA TURAN

Arda Turan ameikacha ofa ya Manchester United ya £29m kwani moyo wa mchezaji huyo unatamani kucheza chini ya kocha wa Chelsea Jose Mourinho. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uturuki anatarajia kuihama Atletico Madrid baada ya klabu hiyo kukubali kupokea ofa ya mchezaji huyo.

BARCELONA - ARDA TURAN

Barcelona wapo kwenye mstari wa mbele kukubaliana na Arda Turan na wasaidizi wake. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uturuki anataka kuondoka Atletico Madrid na usajili wake kwenda Camp Nou unaweka ukawa wazi wiki hii.

MANCHESTER CITY - KEVIN DE BRUYNE

Manchester City hawajakata tamaaa juu ya kumsajiri mchezaji wa Wolfsburg Kevin De Bruyne, licha ya kuuambiwa kwamba hauzwi. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji ana thaman ya £35m lakini mchezaji huyo hajasaini mkataba mpya na klabu yake ya sasa.

EVERTON - SAM BYRAN

Everton tayari wameamua tafuta mbadala wa Seamus Coleman baada ya Manchester United kuonyesha nia ya kumnyakua beki huyo. Toffees wamepanga kumsajiri mchezaji wa Leeds United Sam Byram kama beki huyo ataondoka.

0 comments:

Post a Comment