
Mshambuliaji Emmanuel Okwi ambaye uhamisho wake daima umekuwa ukizungukwa na maswali kila aendako, ameingia katika utata
mwingine baada ya ripoti mpya kudai kwamba alisaini mkataba wa miaka mitano wa kuichezea timu ya SønderjyskE licha ya timu hiyo ya Denmark kutotoa hata senti kwa klabu yake ya Simba.
Utata huo mpya umefuatia Wadenmark hao kutaka kumrejesha Okwi Simba kwa mkopo wa miezi sita baada ya kukwama kuipata leseni yake ya uhamisho ya kimataifa (ITC), ambayo Simba imesema haitaitoa hadi itakapolipwa ada ya uhamisho dola 110,000 (sawa na Sh. milioni 220).

Kumekuwa na mitazamo kwamba kutolewa kwa mkopo kwa Okwi Simba kunaweza kuwa ni janja ya timu hiyo ya Denmark kuvizia Mganda huyo amalize mkataba wake Msimbazi unaomalizika Mei mwakani ili imchukue bure.
Hata hivyo, klabu kubwa kama ya Simba inatarajiwa kwamba ilisaini mkataba na SønderjyskE ambao unaifunga klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Denmark kwamba lazima ilipe deni hilo, hata kama itamleta Msimbazi kwa mkopo.
Taarifa nyingine zinasema kuwa klabu hiyo ya Denmark imefikia uamuzi huo baada ya kumnasa mchezaji mwenye kiwango cha juu zaidi ukilinganisha na Okwi na gharama zake za usajili ni za chini.
Rais wa Simba, Evans Aveva, alisema kwamba kwa sasa wao wanachofuatilia ni kuhakikisha wanalipwa kiasi hicho cha fedha ndipo waruhusu usajili wa njia ya mtandao ufanyike.
Aveva aliweka wazi kwamba, walimuuza Okwi baada ya mchezaji kuangalia maslahi yake na sasa umefika wakati klabu kuhakikisha inapata haki yake na si kuona makosa yaliyofanyika huko nyuma yanajirudia.
Katika uongozi wa Mwenyekiti, Ismail Aden Rage, Okwi aliuzwa kwa klabu ya Etoile du Sahel kwa dau la Dola za Marekani 300,000 lakini fedha hizo hazikulipwa hadi leo na baadaye mshambuliaji huyo alirejea klabu yake ya zamani ya SC Villa na muda mfupi alijiunga na Yanga.
Mganda huyo aliichezea Yanga katika kipindi kifupi na kurejea Simba kwa kueleza kuwa mabingwa hao wa Tanzania Bara hawakutimiza baadhi ya vipengele vilivyoko kwenye mkataba wake.
Chanzo: Mtandao wa IPP Media
Firmino atua Liverpool
Klabu ya Liverpool imekamilisha usajili wa mchezaji wa Hoffenheim Roberto Firmino kwa ada isiyofahamika, huku akitegemea kufanyiwa vipimo vya afya. Mkurugenzi wa Liverpool Ian Ayre alielekea Chile kwa ndege, ambako Firmino anashiriki mashindano ya Copa America ili kumalizia usajili huo unaosadikika kuwa umegharimu euro milioni 40. Baada ya mashindano hayo kumalizika, mchezaji huyo atafanyiwa vipimo vya afya.
Jara aoneshwa mlango wa kutokea baada ya kuchafua hewa
Baada ya kumfanyia mambo machafu mchezaji wa Uruguay Edinson Cavani, mchezaji wa klabu ya Mainz Gonzalo Jara ameambiwa na klabu yake kuwa haitovumilia kitendo hicho na anaweza kutimka klabuni hapo mara tu ofa yoyote itakapopatikana.
Real Madrid yakataa ofa ya Man Utd
Real Madrid wametaa dau la kwanza lililotolewa na klabu ya Manchester Utd kwa ajili ya kumpata beki wa kati wa klabu hiyo Sergio Ramos. Miamba hiyo ya Hispania imepanga kumuuza beki huyo kwa dau la pauni milioni 64 na haitahusisha usajili wa kipa David De Gea kama klabu ya Manchester Utd ilivyokuwa ikihitaji.
Pogba kutua Man City kabla ya Sterling
Manchester City wanataraji kukamilisha usajili wa kiungo mfaransa Paul Pogba. Usajili huo unatazamiwa kukamilika hata kabla ya usajili wa winga wa Liverpool Raheem Sterling.
Cech ndani, Ospina nje Arsenal
Klabu ya Arsenal inaweza kumuuza golikipa wake David Ospina licha ya kufanya vema mzunguko wa pili wa msimu uliopita. Klabu ya Fenerbahce imeonesha nia kubwa ya kumuwania kipa huyo huku kipa aliyeonekana kusuasua mara kwa mara Wojciech Szczesny akitegemewa kuwa msaidizi wa Petr Cech.
FUMBO KWA SIMBA, OKWI KUREJESHWA KWA MKOPO...
Popular Posts
-
Mchezaji wa zamani wa klabu ya Real Madrid Ramon Calderon anafikiria kuwa klabu ya Manchester United itakuwa imetumia hekima kumsajili Ser...
-
ARSENAL INA MATUMAINI YA KUMNASA BENZEMA: Azma ya Arsenal kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema imepata mwamko mpya baada ...
-
KIIZA APEWA WIKI MBILI KUONGEZA KIWANGO
-
Chile imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Copa America baada ya kuichapa Uruguay 1-0, lakini mapema kipindi cha pili mshambuliaji...








0 comments:
Post a Comment