RAMOS KUPEWA MIAKA MITANO UNITED,TURAN KUTUA NOU CAMP,DAU LAPANDA KWA MRITHI WA CECH,PSG WATENGA €60M KWA DI MARIA........NA NYINGINE ZA ULAYA ZILIZOJILI LEO........

Thursday, 2 July 2015

MANCHESTER UNITED - RAMOS,SCHWEINSTEIGER,SCHNEIDER & DE GEA

Manchester United imepanga kumpa mkataba wa miaka mitano Sergio Ramos wenye thamani ya €55m (£39m) ukitoa kodi,mchezaji huyo wa kimataifa wa Hisapania hayupo tayari kubaki Bernabeu.


Manchester United wataikosa huduma ya Bastian Schweinsteiger kwani mchezaji huyo anatarajia kukaa katika klabu yake ya Bayern mpaka mkataba wake utakapoisha 2016.


Ofa ya £20 iliyokuwa imetolewa na Manchester United kwa Morgan Schneiderlin imepigwa chini na Southampton.


Manchester United hawajapokea ofa yeyote kutoka Real Madrid kwa ajili ya David De Gea na bado wamesimamia €50m (£35.4m) kwa ajili ya golikipa huyo.


REAL MADRID - FERNANDO LLORENTE

Bosi wa Real Madrid Rafa Benitez anatarajia kumsajili Fernando Llorente ambaye anatarajia kuihama klabu yake ya Juventus msimu huu, mchezaji huyo anahitaji kujiimalisha na kubaki na ubora wake.


BARCELONA - ARDA TURAN

Barcelona wamejipanga kufanya usajili wa nguvu msimu huu, baada ya kufikia makubaliano ya €35m pamoja na motisha kwa nyota wa Atletico Madrid Arda Turan.

Barcelona watakuwa wameipiku klabu ya chelsea ambayo awali ilitangaza kutoa £29(€40.9) bila kuweka motisha kwa mchezaji huyo.


CHELSEA - LOIC REMY & ASMIR BEGOVIC

Chelsea wameamua kuachana na mpango wa kumuuza mshambuliaji Loic Remy msimu huu. West Ham walikuwa wanaongoza mbio za kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa kwa ada ya £15m  lakini Jose Mourinho ameonyesha kumhitaji mchezaji huyo.


Jose Mourinho ameongeza dau kwa ajili ya kumsajili golikipa wa Stoke City Asmir Begovic, golikipa huyo ataigharimu Chelsea ada inayosadikiwa kuwa £8. mchezaji huyo wa kimataifa wa Bosnia anatamani kuelekea  Stamford Bridge.

MANCHESTER CITY - KEVIN DE BRUYNE & KARIM BELLARABI

Klabu ya Manchester City imekalibia kumnyakua Kevin De Bruyne na watakutana na wakala wa kiungo huyo wiki ijayo.


Manchester City wamejipanga kutoa kitita cha €35 kwa ajili ya winga wa Bayer Leverkusen Karim Bellarabi.

AC MILAN & INTER - MARIO SUAREZ & MATIJA NASTASIC

AC Milan na Inter wapo kwenye mbio za kumsajili kiungo wa Atletico Madrid Mario Suarez.


AC Milan wameamua kumfungia kazi upya beki wa kati wa Schalke Matija Nastasic.

JUVENTUS - OSCAR

Juventus wako tayari kutumia €28(£19.8m) kwa ajili ya kumsajili Oscar kutoka Chelsea.

ATLETICO MADRID - JUAN CUADRADO,MIRALEM  PJANIC & FILIPE LUIS

Atletico Madrid wamejiunga na Inter pamoja na Juventus katika mbio za kumnyakua winga wa Chelsea Juan Cuadrado.


Klabu ya Atletico Madrid imepania kunasa saini ya  Miralem Pjanic, lakini hawajafikia dau ambalo klabu yake ya Roma imafikia ambayo ni €45m kwa ajili ya kiungo huyo.


Chelsea wameitaka klabu ya Atletico Madrid kulipa €20 kwa ajili ya Filipe Luis

PSG - DI MARIA & PEDRO RODRIGUEZ

klabu ya PSG inatarajia kutoa kitita cha €60m kwa ajili ya winga wa Manchester United Angel Di Maria. Ofa hiyo inatarajiwa kutolewa leo.


Pia klabu hiyo wanaangalia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Pedro Rodriguez

0 comments:

Post a Comment