WAWA WA AZAM FC AIBUKA KINARA WA MCHEZO MECHI DHIDI YA MALAKIA YA SUDANI KUSINI...

Tuesday, 21 July 2015

wawa siku alipotambulishwa na Azam

Wawa aliyetua Azam msimu uliopita akitokea El Merreikh ya Sudan amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha kocha Stewart Hall

BEKI wa kati raia wa Ivory Coasty Pascal Wawa leo ameibuka mchezaji bora katika mechi ambayo timu yake ya Azam imeifunga Malakia ya Sudan Kusuni mabao 2-0, ukiwa ni ushidi wa pili mfululizo kwenye michuano ya Kombe la Kagame inayofanyika Dar es Salaam.

Wawa aliyetua Azam msimu uliopita akitokea El Merreikh ya Sudan amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha kocha Stewart Hall raia wa Uingereza kiasi cha kumfanya abigiwe makofi kila anapocheza.

“Nafurahi kupata tuzo hii lakini lengo kubwa la jitihada zangu ni kufuata vizuri maelekezo ya kocha pamoja na kutumia uwezo wangu kuipa mafanikio Azam,”amesema Wawa.

Wawa amesema angependa kuona taji hilo akilichukua kwa mara ya bili baada ya mwaka jana kufanya hivyo nchini Rwanda akiwa na El Merreikh na anaamini hilo linawezekana kutokana na ubora wa kikosi chao cha msimu huu.

0 comments:

Post a Comment