WOJCIECH SZCZESNY KUJIUNGA NA ROMA KWA MKOPO...

Wednesday, 22 July 2015

Szczesny to join Roma on loan

Mlinda mlango wa klabu ya Arsenal Wojciech Szczesny yupo kwenye harakati za kujiunga na klabu ya Roma kwa mkopo, mtandao wa Goal umetanabaisha.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Poland alipoteza nafasi yake kwa David Ospina mzunguko wa pili wa msimu uliopita wa Ligi Kuu 2014-2015, japokuwa aliichezea Arsenal michezo sita ya FA na kuipatia klabu hiyo kombe hilo mara mbili mfululizo.

Mapema majira haya The Gunners walimsajili Petr Cech kutoka Chelsea kwa ada inayokaribia pauni milioni 11, dili lililosifiwa na wengi kuwa ni wakati wa kilabu hicho kinachonolewa na Arsene Wenger kunyakuwa tena taji kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2004.

Kwa sasa Wenger ameamua kuwa ni Szczesny ndiye atakayeondolewa katika kikosi hicho kuelekea katika kampeni mpya, huku Ospina na Damian martinez wakibakia kutoa upinzani kwa Cech.

Bosi huyo wa The Gunners anaamini kuwa Martinez mwenye umri wa miaka 22, ambaye alisajiliwa kutoka Independiente mwaka 2010, atakuwa tishio katika kilabu hicho hapo baadaye.

Msimu uliopita aliwahi kumjumuisha mlinda mlango huyo wa Kiargentina akidai kuwa kulikuwa na makipa watatu wenye viwango vya dunia "world class" katika vitabu vya Arsenal pale Emirates, msimamo ambao ameutoa walipokuwa wakishiriki Asia Trophy wiki iliyopita.

Imeripotiwa kuwa klabu ya Roma italipa euro 400,000 (pauni 281,000) kwa ajili ya kumchukua kwa mkopo, na watakuwa na fursa ya kufanya dili la kudumu.

Szczesny alikamatwa akivuta sigara kwenye chumba cha kubadilishia nguo kufuatia kipigo kutoka kwa kilabu cha Southampton mwishoni mwa mwaka, huku kukiwa na tetesi za Wenger kukataa kumkacha katika kikosi chake kutokana na matokeo, hakupata tena nafasi kutokea Ligi Kuu mzunguko wote wa pili wa msimu uliopita.

Katika kipindi cha miezi ya mwisho ya kampeni ya 2014-2015 alipokea wito kutoka kwa walinda mlango wa zamani wa Poland Jan Tomaszewski na Jerzy Dudek kujiondoa klabuni hapo, na kabla ya ushindi wa Kombe la FA dhidi ya Aston Villa, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alilazimishwa na baba yake kujiweka mbali na ukosoaji wa Wenger.

Kwa sasa ataelekea Roma, ambapo Morgan De Sanctis mwenye umri wa miaka 38 alitokea mara 35 kwenye Ligi msimu uliopita.

Giallorossi walimaliza nafasi ya pili katika Serie A msimu uliopita wa mwaka 2014-2015, pointi 17 nyuma ya mabingwa Juventus.

0 comments:

Post a Comment