YALIYOJIRI KWENYE ANGA ZA USAJILI BARANI ULAYA...

Monday, 20 July 2015

"POGBA HAUZWI HATA KWA EURO 100 MILIONI"-JUVENTUS:



Klabu ya Juventus imetanabaisha kuwa kiungo wao Paul Pogba hauzwi kwa bei yoyote majira haya na hawapo tayari kukubali ofa yoyote hata kama ni euro milioni 100.

Chanzo: La Stampa
Jumatatu, 7/20/2015 06:45

WALCOTT ANATAKA MSHAHARA WA PAUNI 100,000 KWA WIKI:



Mwaka 2013 Theo Walcott alitia saini mkataba wa pauni 90,000 kwa wiki lakini anahisi kwamba anastahili kulipwa sawa na wachezaji wa Arsenal wanaopokea mkwanja mrefu, huku mazungumzo yakiendelea.

Chanzo: The Guardian
Jumatatu, 7/20/2015 00:12

ASTON VILLA INAMUWANIA ADEBAYOR KUZIBA PENGO LA BENTEKE:



Tim sherwood anatazamia kuungana tena na mshambuliaji wa Tottenham Emmanuel Adebayor kama mbadala wa Christian Benteke katika klabu ya Aston Villa, lakini mshahara wa pauni 100,000 kwa wiki utathibitisha kikwazo.

Chanzo: Mirror
Jumapili, 7/19/2015 23:18

EVERTON WATOA TAMKO KUHUSU KUMUUZA STONE KWA CHELSEA:



Everton wamefikia hatua ya kutoa msimamo wao kwa maandishi kuhusu kumuuza mchezaji wao John Stones kwa kukataa dau la pauni milioni 20 lililotolewa na Chelsea, wakielezea kwa kina kukataa kwao kumuuza.

Chanzo: Daily Express
Jumapili, 7/19/2015 23:10

CHELSEA KUMUUZA CUADRADO:



Jose Mourinho amefungua milango kwa timu zinazomuhitaji Juan Cuadrado, huku mchezaji huyo akipambana kutulia katika klabu hiyo, lakini watakubali ofa itakayoendana na euro 33 milioni iliyotumika kwa winga huyo katika dirisha dogo la usajili la mwezi wa kwanza.

Chanzo: The Guardian
Jumapili, 7/19/2015 22:25

MAN UTD YAMUONGEZA ROMERO KWENYE LISTI YA MAKIPA INAYOWAHITAJI:



Sergio Romero, ambaye ni mchezaji huru baada ya kutimka Sampdoria, yupo kwenye listi fupi ya makipa ambao wanawaniwa na klabu ya Manchester United kama mbadala wa David De Gea , pamoja pia na mlinda mlango wa Ajax Jasper Cillessen, kama mlinda mlango huyo atatimkia Real Madrid majira haya.

Chanzo: Daily Mirror
Jumapili, 7/19/2015 21:26

MITROVIC AKWEA PIPA KUKAMILISHA USAJILI WAKE NEWCASTLE:



Mshambuliaji wa Anderlecht Mitrovic anatazamiwa kukamilisha usajili wa pili wa klabu ya Newcastle wenye gharama ya pauni milioni 11.5, akipokea mshahara wa pauni 33,000 kwa wiki pamoja na pauni 16,000 kwa kila mchezo atakaocheza wakashinda.

Chanzo: Daily Mirror
Jumapili, 7/19/2015 20:53

GALATASARAY WANAMUWANIA FLAMINI:



Klabu ya Galatasaray inaimani kuwa itakamilisha dili la kumnyakuwa Mathieu Flamini wiki hii, huku Arsenal wakiwa na furaha ya kupokea mshiko kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31, ambaye amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake.

Chanzo: Daily Mirror
Jumapili, 7/19/2015 20:11

TOTTENHAM IMEINGIA KWENYE MBIO ZA KUMUWANIA CHICHARITO:



Kocha wa Spurs Mauricio Pochettino anamnyatia mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Javier Hernandez ili kuongeza kasi ya ushambuliaji katika kikosi chake, lakini kuondoka kwa Robin van Persie kunaweza kumpatia nafasi mshambuliaji huyo wa Mexico pale Old Trafford msimu unaokuja.

Chanzo: gianlucadimarzio.com
Jumapili, 7/19/2015 19:44

0 comments:

Post a Comment