
Wayne Rooney atinga tena uzi wa Everton kwa mara ya kwanza tangu aihame klabu hiyo mwaka 2004 walipokipiga dhidi ya Villarreal ambapo alishuhudia timu hiyo ikila kichapo cha 2-1 kwenye mchezo wa heshima ya Duncan Ferguson.
Mapokezi ya Rooney yaliambatana na shangwe pamoja na kuzomewa kutoka kwa mashabiki wa nyumbani-wengi wamedhihirisha kuwa hawakufurahishwa na kitendo cha mchezaji huyo kutimka klabuni hapo na kujiunga na Manchester United mnamo mwaka 2004-wakati Ferguson alikaribishwa kwa furaha sana.

Wachezaji hao wawili waliwahi kukipiga pamoja katika kikosi cha kwanza cha kilabu hicho wakati Rooney alipoingia kikosi cha kwanza mwaka 2002, lakini walishindwa kuipa timu hiyo ushindi baada ya Gerard na Matias Nahuel kuipatia Villarreal mabao mawili.
Katika mchezo huo Rooney alikipiga kwa dakika 16 za mwisho na kupokelewa kwa taswira tofauti kutoka kwa mashabiki wa Goodison Park.

Firmino atua Liverpool
Klabu ya Liverpool imekamilisha usajili wa mchezaji wa Hoffenheim Roberto Firmino kwa ada isiyofahamika, huku akitegemea kufanyiwa vipimo vya afya. Mkurugenzi wa Liverpool Ian Ayre alielekea Chile kwa ndege, ambako Firmino anashiriki mashindano ya Copa America ili kumalizia usajili huo unaosadikika kuwa umegharimu euro milioni 40. Baada ya mashindano hayo kumalizika, mchezaji huyo atafanyiwa vipimo vya afya.
Jara aoneshwa mlango wa kutokea baada ya kuchafua hewa
Baada ya kumfanyia mambo machafu mchezaji wa Uruguay Edinson Cavani, mchezaji wa klabu ya Mainz Gonzalo Jara ameambiwa na klabu yake kuwa haitovumilia kitendo hicho na anaweza kutimka klabuni hapo mara tu ofa yoyote itakapopatikana.
Real Madrid yakataa ofa ya Man Utd
Real Madrid wametaa dau la kwanza lililotolewa na klabu ya Manchester Utd kwa ajili ya kumpata beki wa kati wa klabu hiyo Sergio Ramos. Miamba hiyo ya Hispania imepanga kumuuza beki huyo kwa dau la pauni milioni 64 na haitahusisha usajili wa kipa David De Gea kama klabu ya Manchester Utd ilivyokuwa ikihitaji.
Pogba kutua Man City kabla ya Sterling
Manchester City wanataraji kukamilisha usajili wa kiungo mfaransa Paul Pogba. Usajili huo unatazamiwa kukamilika hata kabla ya usajili wa winga wa Liverpool Raheem Sterling.
Cech ndani, Ospina nje Arsenal
Klabu ya Arsenal inaweza kumuuza golikipa wake David Ospina licha ya kufanya vema mzunguko wa pili wa msimu uliopita. Klabu ya Fenerbahce imeonesha nia kubwa ya kumuwania kipa huyo huku kipa aliyeonekana kusuasua mara kwa mara Wojciech Szczesny akitegemewa kuwa msaidizi wa Petr Cech.
ROONEY AREJEA TENA EVERTON TANGU ATIMKIE MAN UTD MWAKA 2004...
Popular Posts
-
Mchezaji wa zamani wa klabu ya Real Madrid Ramon Calderon anafikiria kuwa klabu ya Manchester United itakuwa imetumia hekima kumsajili Ser...
-
ARSENAL INA MATUMAINI YA KUMNASA BENZEMA: Azma ya Arsenal kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema imepata mwamko mpya baada ...
-
KIIZA APEWA WIKI MBILI KUONGEZA KIWANGO
-
Chile imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Copa America baada ya kuichapa Uruguay 1-0, lakini mapema kipindi cha pili mshambuliaji...








0 comments:
Post a Comment