ARGENTINA YA MESSI YATOA SARE, UJERUMANI YAUA SABA, LEWANDOWSKI APIGA TATU NDANI YA DAKIKA NNE...

Sunday, 14 June 2015




Timu ya taifa ya Argentina imeanza kwa sare michuano ya Copa America inayoendelea nchini Chile baada ya usiku wa kuamkia leo kutoka 2-2 dhidi ya Paraguay.

Watu wengi walidhani Argentina ingeibuka na ushindi baada ya Sergio Aguero kufunga goli la kuongoza dakika ya 29, kabla ya Lionel Messi kutumbukiza kitu kambani dakika ya 36.
Messi amefunga goli hilo kwa mkwaju wa penalti uliotokana na beki wa Paraguay, Miguel Samudio kumuangusha kwenye eneo la hatari Angel di Maria.
Hadi timu zinakwenda mapumziko, Argentina walikuwa wanaongoza 2-0.

Kipindi cha pili mambo yalibadilika, Paraguay walifunga goli la kwanza dakika ya 60′ kupitia kwa Nelson Valdez na wakasawazisha dakika ya 90 kupitia kwa nyota wa Spartak Moscow, Lucas Barrios.

Mechi nyingine ya kundi B imeshuhudiwa Uruguay ikishinda goli 1-0 dhidi ya Jamaica.
Goli pekee la Uruguay limefungwa dakika ya 52 kupitia kwa Cristian Rodriguez.

The man of the moment Schurrle celebrates with his team-mates having completed a hat-trick

Magoli matatu "Hat-Trick" yaliyotupiwa nyavuni dakika ya 28, 65, na 71 na mshambuliaji Andre Schurrle wa timu ya Taifa ya Ujerumani yaliiweka Gibraltar kwenye upanga wa magoli 7-0 katika mashindano ya kuwania kufuzu Euro 2016.

Magoli mengine yaliyoshuhudiwa yaliwekwa kimiani na Max Kruse dakika ya 47 na 81, Ilkay Gundogan dakika ya 51, na Karim Bellarabi dakika 57.

Timu hiyo ya taifa ya Ujerumani iliyokuwa inatumia mfumo wa 3-1-4-2 iliibuka na ushindi wa magoli 7-0 huku kiungo wa Arsenal Mesut Ozil akitoa pasi tatu za magoli hayo.



Mechi nyingine imeshuhudiwa Poland ikiibuka na ushindi wa mabao 4-0 baada ya mshambuliaji wao Robert Lewandowski kutupia magoli matatu "Hat-Trick" ndani ya dakika nne tu.

Robert Lewandowski kwa sasa anaongoza katika safu ya wafungaji akiwa na jumla ya magoli saba na kuisaidia timu yake ya taifa kushikilia usukani wa kundi D.

0 comments:

Post a Comment