
Klabu ya Manchester United ipo tayari kutumia kitita cha Euro milioni 27.5 kumsajili beki wa Real Madrid Sergio Ramos. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania amekataa kufanya mazungumzo ya mkataba mpya na miamba hao wa La Liga sababu ikiwa ni klabu hiyo kutokukidhi mahitaji yake ya mshahara. Klabu nyingine zinazomuwania mchezaji huyo ni Manchester City na Chelsea.
Baada ya uwezekano wa kumleta mjini Manchester beki wa kati wa Borussia Dortmund Mat Hummels kugonga miamba mara kadhaa, klabu ya Manchester United sasa imeelekeza macho yake kwa mchezaji wa Valencia Nicolas Otamendi na ipo tayari kutoa dau la Euro milioni 50 kumnasa mchezaji huyo.

Arsenal wamekata tamaa ya kumsajili mchezaji wa klabu ya Liverpool Raheem Sterling kutokana na mchezaji huyo kuuzwa bei ghali. Kwa sasa washika bunduki hao wana nia ya kuimarisha kikosi chao katika safu ya kiungo na golini kwa hiyo hawapo tayari kumtumia mchezaji wao Theo Walcott kama sehemu ya mpango wa kumpata Raheem Sterling.

Klabu ya PSG ina mpango wa kutoa upinzani kwa klabu ya Arsenal kwa ajili ya kumuwania golikipa wa klabu ya Chelsea Petr Cech. Klabu hiyo ya Chelsea "The Blues" itamruhusu mlinda mlango huyo kujiunga na timu pinzani za Uingereza zikiwemo Arsenal na Manchester United.

Firmino atua Liverpool
Klabu ya Liverpool imekamilisha usajili wa mchezaji wa Hoffenheim Roberto Firmino kwa ada isiyofahamika, huku akitegemea kufanyiwa vipimo vya afya. Mkurugenzi wa Liverpool Ian Ayre alielekea Chile kwa ndege, ambako Firmino anashiriki mashindano ya Copa America ili kumalizia usajili huo unaosadikika kuwa umegharimu euro milioni 40. Baada ya mashindano hayo kumalizika, mchezaji huyo atafanyiwa vipimo vya afya.
Jara aoneshwa mlango wa kutokea baada ya kuchafua hewa
Baada ya kumfanyia mambo machafu mchezaji wa Uruguay Edinson Cavani, mchezaji wa klabu ya Mainz Gonzalo Jara ameambiwa na klabu yake kuwa haitovumilia kitendo hicho na anaweza kutimka klabuni hapo mara tu ofa yoyote itakapopatikana.
Real Madrid yakataa ofa ya Man Utd
Real Madrid wametaa dau la kwanza lililotolewa na klabu ya Manchester Utd kwa ajili ya kumpata beki wa kati wa klabu hiyo Sergio Ramos. Miamba hiyo ya Hispania imepanga kumuuza beki huyo kwa dau la pauni milioni 64 na haitahusisha usajili wa kipa David De Gea kama klabu ya Manchester Utd ilivyokuwa ikihitaji.
Pogba kutua Man City kabla ya Sterling
Manchester City wanataraji kukamilisha usajili wa kiungo mfaransa Paul Pogba. Usajili huo unatazamiwa kukamilika hata kabla ya usajili wa winga wa Liverpool Raheem Sterling.
Cech ndani, Ospina nje Arsenal
Klabu ya Arsenal inaweza kumuuza golikipa wake David Ospina licha ya kufanya vema mzunguko wa pili wa msimu uliopita. Klabu ya Fenerbahce imeonesha nia kubwa ya kumuwania kipa huyo huku kipa aliyeonekana kusuasua mara kwa mara Wojciech Szczesny akitegemewa kuwa msaidizi wa Petr Cech.
MANCHESTER UNITED YAMUWANIA SERGIO RAMOS, ARSENAL KUMKOSA RAHEEM STERLING...
Popular Posts
-
Mchezaji wa zamani wa klabu ya Real Madrid Ramon Calderon anafikiria kuwa klabu ya Manchester United itakuwa imetumia hekima kumsajili Ser...
-
ARSENAL INA MATUMAINI YA KUMNASA BENZEMA: Azma ya Arsenal kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema imepata mwamko mpya baada ...
-
KIIZA APEWA WIKI MBILI KUONGEZA KIWANGO
-
Chile imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Copa America baada ya kuichapa Uruguay 1-0, lakini mapema kipindi cha pili mshambuliaji...








0 comments:
Post a Comment