BOLT: SIMUOGOPI GATLIN....

Friday, 12 June 2015



Usain Bolt, mwana riadha mwenye kasi kubwa zaidi duniani, ameonekana kuachia nafasi yake baada ya kukumbwa na majeraha mwaka 2014, wakati mwanariadha mwingine Gatlin akiweka rekodi ya mwaka ya mwanaraidha mwenye kasi na kutangaza kwamba anaweza kumshinda mkongwe huyo.

"Gatlin amekuwa akiongea sana, na kuzungumza mengi" alizungumza Bolt kabla ya mashindano ya adidas Grand Prix katika kisiwa cha Randall.

"Ameweza kudhihirisha kwamba ana kasi na yupo tayari. Kwahiyo itakuwa ni shauku kubwa kuingia katika Mashindano ya Dunia."

"Natarajia zaidi kushindana na majadiliano ya watu...kwa sababu kama hutoyashinda, utaonekana mjinga."

Justin Gatlin: This season's fastest man so far

Gatlin, ambaye alifungiwa kushiriki michuano miwili kufuatia shutuma za kutumia madawa ya kuongeza nguvu, mwezi uliopita alikimbia kwa sekunde 9.74-rekodi ya kipekee na ya kasi katika mita 100 mwaka 2015 mjini Doha na kuongoza kwa sekunde 19.68 kwenye michuano ya mita 200 mjini Eugene siku 15 baadae.

Bolt, ambaye anashikilia rekodi ya Dunia katika matukio yote (sekunde 9.58 mita 100 na sekunde 19.19 mita 200), atakimbia mita 200 tu siku ya Jumamosi huku akiendelea kuamsha hisia kwa mashabiki juu ya ushindani utakaoonesha dhidi ya Gatlin.

Hata hivyo Mjamaika huyo amesisitiza uteuzi wake wa mbio hauna uhusiano wowote wa woga dhidi ya wanariadha wengine.

"Hofu?, huwa nacheka nikisikia watu wakisema hivyo, nimekuwa katika mchezo huu kwa miaka sasa, na sijawahi kumkwepa yeyote, inapohitajika siku zote huwa natokea nakuthibitisha mimi ni bora," alisema Bolt.

"Ukweli ni kwamba, sipo katika ubora wangu kwa sasa na sitojitokeza tu kama ninajua ndio nimerudi na nina hitaji muda kufikia pale ninapohitaji."

"Nitakapofika Beijing, nitakuwa tayari na hapo ndipo mmpambano utakuwepo."

Bolt alisema, shauku iliyopo baina ya wakimbiaji wa mbio fupi inaweza leta hamasa kubwa katika Mashindano ya Dunia.

"watu huwa wanakuwa na hamu ya mashindano. Nini kitatokea?," alisema.

"Justin ni mkimbiaji mzuri, Tyson ni mkimbiaji mzuri, Asafa ni mkimbiaji mzuri, Usain ni mkimbiaji mzuri."

"Tutakapofika kwenye mashindano, itakuwa kama mlipuko."


0 comments:

Post a Comment