MADRID YAMTAKA KONDOGBIA, PSG YAMFUNGIA KAZI PEDRO NA REMY ARUHUSIWA KUZUNGUMZA NA WEST HAM....

Friday, 12 June 2015



Klabu ya Real Madrid inamuwania kiungo wa Monaco Geoffrey Kondogbia.

Klabu hiyo ya Ufaransa inahitaji angalau dau la Euro milioni 35 kumuuza mchezaji huyo.

Klabu ya Arsenal ni miongoni mwa vilabu vikubwa vinavyowania saini ya kiungo huyo.


PSG YAMTAKA PEDRO...



Miamba ya Ufaransa PSG ina nia ya kumsajili winga wa Barcelona Pedro Rodriguez, ingawa winga huyo hivi karibuni alisaini mkataba mpya na miamba hao walionyakua taji la Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.
Hata hivyo klabu ya PSG bado inaonesha nia ya kuendelea kumshawishi winga huyo ajiunge nao.

REMY APEWA RUHUSA KUONGEA NA WESTHAM...



Mabingwa wa ligi ya Uingereza Chelsea ("The Blues") wamemruhusu mshambuliaji wao Loic Remy kufanya mazungumzo na klabu ya West Ham kuhusiana na usajili.

Mshambuliaji huyo ameonesha nia ya kutaka kutimka klabuni hapo baada ya kocha huyo wa Upton Park kuonesha nia ya kumuhitaji.

0 comments:

Post a Comment