CABAYE: "NATAKA KUCHEZA KILA WIKI..."

Tuesday, 9 June 2015

I need to play every week, insists Cabaye


Kiungo wa PSG Yohan Cabaye ametoa tamko kali kwamba atawahama mabingwa hao wa Ligue 1 na kwenda kukipiga katika klabu nyingine msimu ujao.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa alijiunga na miamba hiyo akitokea klabu ya Newcastle United mwanzoni mwa mwaka 2014 na kufanikiwa kushinda mataji mawili, medali ya Coupe de la Ligue na Coupe de France wakati wa muda wake mjini Paris.

Lakini kiungo huyo kwa kiasi kikubwa amekuwa mchezaji wa akiba chini ya kocha mkuu Laurent Blanc, na kufanikiwa kuanza mechi 22 za Ligue 1.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amekuwa akihusishwa kuungana na kocha wake wa zamani wa Newcastle United Alan Pardew ambaye kwa sasa anaifundisha klabu ya Crystal Palace.

"Kuna hali sasa ambapo sikuwa na muda wa kucheza kama nilivyotegemea" aliiambia Infosport+.

"Wawakilishi wangu wanatafuta ufumbuzi sahihi. Katika siku zijazo, jambo muhimu ni kucheza kila mwisho wa wiki."

Alipoulizwa kuhusu kurudi Ligi Kuu ya Uingereza, Cabaye aliongeza: [Ni] Ligi ninayoipenda, nchi pia.

"Kunaweza kuwa na nafasi, kama kunaweza kuwa na watu wengine. Jambo muhimu ni kwamba nitafikiria kwa makini na kufanya maamuzi sahihi."

0 comments:

Post a Comment