REAL SOCIEDAD YAMKARIBISHA JOEL CAMPBELL

Wednesday, 10 June 2015



Raisi wa Real Sociedad Jokin Aperribay amethibitisha kuwa klabu hiyo ina mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Joel Campbell.


Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alitumia nusu ya msimu uliopita kwa mkopo katika klabu ya Villarreal baada ya kushindwa kupata namba katika kikosi cha kwanza cha Arsene Wenger.

Campbell alijiunga na Arsenal mnamo mwaka 2011 lakini amefanikiwa kucheza mechi 10 tu katika klabu hiyo. Alipelekwa kwa mkopo katika klabu za Lorient, Real Betis na Olympiakos, na sasa klabu ya Real Sociedad imeonesha nia ya kumsajili mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Costa Rica.

"Ni mchezaji mwenye kuvutia, lakini hivi sasa hakuna majadiliano ya uhamisho," Aperribay aliiambia Teledonosti.

"Tunahitaji kuchambua hali ya kifedha ambayo uhamisho huu utagharimu."

0 comments:

Post a Comment