CASILLAS KUTUA ARSENAL

Wednesday, 10 June 2015



Kocha wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger anafuatilia kwa ukaribu maendeleo ya kipa wa Real Madrid Iker Casillas ambaye anataka kutimka klabuni hapo kufuatia taarifa za klabu hiyo kuwa katika mazungumzo ya mwisho na kipa wa klabu ya Manchester United David De Gea.

Bosi huyo wa Arsenal angependelea kuipata saini ya kipa wa Chelsea Petr Cech lakini badala yake anaweza kumchukua Mhispania huyo kama ataondoka katika klabu yake ya sasa ya Real Madrid.

Kwa sasa nahodha huyo wa Madrid ameamua kuondoka katika klabu hiyo ili kujitafutia namba katika kikosi cha kwanza mahala pengine.

0 comments:

Post a Comment