MARTA VIEIRA DA SILVA AWEKA REKODI YA KUPACHIKA MABAO KOMBE LA DUNIA

Wednesday, 10 June 2015




Mshambuliaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Brazil Marta Vieira da Silva maarufu kama Marta ameweka historia ya kuwa mfungaji bora wa michuano ya kombe la dunia la wanawake baada ya kufikisha mabao 15.

Marta mwenye umri wa miaka 29, amefikisha idadi ya mabao hayo baada ya kufunga bao moja kwa mkwaju wa penati kwenye mchezo wa timu yake dhidi ya korea kusini ambapo Brazili waliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 2-0.

Ushindi huo umeifanya Brazil kuwa vinara wa kundi E, Baada ya Hispania na Costa Rica kwenda sare ya kufungana 1-1.

Mshambuliaji huyu ameichezea timu ya taifa jumla ya michezo 137 akiwa kafunga mabao 93. Kwa sasa Marta ni mchezaji wa klabu ya Rosengard FC ya Sweden.

0 comments:

Post a Comment