DE GEA: NATAKA KWENDA REAL MADRID...

Tuesday, 9 June 2015




David De Gea ameitaarifu klabu yake ya Manchester United kwamba atatimka klabuni hapo na kujiunga na miamba ya hispania Real Madrid.

Klabu ya Manchester United (Mashetani Wekundu) wanaweza kuamua kumuuza au kubaki na kipa huyo mpaka mkataba wake klabuni hapo utakapomalizika mwishoni mwa msimu ujao na hivyo kuondoka kama mchezaji huru.

Kuamua kuondoka klabuni hapo kumeletwa na sababu kadhaa ikiwemo ya yeye kutaka kurudi kwao ili akaishi na mpenzi wake ambae bado anaishi huko. Pia kipa huyo anatamani kufuata nyayo za nyota nguli waliondoka klabuni hapo na kujiunga na miamba hiyo ya hispania miaka kadhaa iliyopita.

Nyota hao ni pamoja na Cristiano Ronaldo, Ruud Van Nistelrooy, Gabriel Heinze na David Beckham.



Kama Kipa huyo atatimka klabuni hapo, kocha wa mashetani hao Louis Van Gaal atahakikisha anaipata saini ya kipa wa Uholanzi Jasper  Cillessen aliyefanya nae kazi katika timu ya taifa.


0 comments:

Post a Comment