
Kutoka Aaron Ramsey aliyeifungia Arsenal katika hatua ya makundi dhidi ya Galatasaray hadi kwa Ivan Rakitic aliyeifungia Barcelona goli la kuongoza katika fainali dhidi ya Juventus, mabao yaliyofungwa msimu huu wa Ligi ya Mabingwa Ulaya yameleta msisimko wa aina yake tangu mwanzo hadi mwisho.
Juhudi bora zilizofanyika katika ufungaji wa magoli hayo zimepigiwa kura kuwania goli la Wiki la Ligi ya Mabingwa Ulaya, yaliyowasilishwa na Nissan. Sasa ni wakati wa kuamua goli bora la mashindano yote.
Wachezaji wanaowania kinyang'anyilo hicho kutoka Nissan ni:
1. Aaron Ramsey Vs Galatasaray
Galatasaray 1 - 4 Arsenal
2. Branislav Vs PSG
PSG 1 - 1 Chelsea
3. Leroy Sane Vs Real Madrid
Real Madrid 3 - 4 Schalke 04
4. Luis Suarez Vs PSG
PSG 1 - 3 Barcelona
5. Lionel Messi Vs Bayern
Barcelona 3 - 0 Bayern
6. Ivan Rakitic Vs Juventus
Juventus 1 - 3 Barcelona
Pigia kura bao la ushindi katika mashindano haya ya goli la Wiki yanayowasilishwa na Nissan na unaweza kushinda zawadi ya kipekee ya mpira uliotumika katika mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2014/2015.
Piga kura yako hapa:
http://bit.ly/1wucePX
Firmino atua Liverpool
Klabu ya Liverpool imekamilisha usajili wa mchezaji wa Hoffenheim Roberto Firmino kwa ada isiyofahamika, huku akitegemea kufanyiwa vipimo vya afya. Mkurugenzi wa Liverpool Ian Ayre alielekea Chile kwa ndege, ambako Firmino anashiriki mashindano ya Copa America ili kumalizia usajili huo unaosadikika kuwa umegharimu euro milioni 40. Baada ya mashindano hayo kumalizika, mchezaji huyo atafanyiwa vipimo vya afya.
Jara aoneshwa mlango wa kutokea baada ya kuchafua hewa
Baada ya kumfanyia mambo machafu mchezaji wa Uruguay Edinson Cavani, mchezaji wa klabu ya Mainz Gonzalo Jara ameambiwa na klabu yake kuwa haitovumilia kitendo hicho na anaweza kutimka klabuni hapo mara tu ofa yoyote itakapopatikana.
Real Madrid yakataa ofa ya Man Utd
Real Madrid wametaa dau la kwanza lililotolewa na klabu ya Manchester Utd kwa ajili ya kumpata beki wa kati wa klabu hiyo Sergio Ramos. Miamba hiyo ya Hispania imepanga kumuuza beki huyo kwa dau la pauni milioni 64 na haitahusisha usajili wa kipa David De Gea kama klabu ya Manchester Utd ilivyokuwa ikihitaji.
Pogba kutua Man City kabla ya Sterling
Manchester City wanataraji kukamilisha usajili wa kiungo mfaransa Paul Pogba. Usajili huo unatazamiwa kukamilika hata kabla ya usajili wa winga wa Liverpool Raheem Sterling.
Cech ndani, Ospina nje Arsenal
Klabu ya Arsenal inaweza kumuuza golikipa wake David Ospina licha ya kufanya vema mzunguko wa pili wa msimu uliopita. Klabu ya Fenerbahce imeonesha nia kubwa ya kumuwania kipa huyo huku kipa aliyeonekana kusuasua mara kwa mara Wojciech Szczesny akitegemewa kuwa msaidizi wa Petr Cech.
PIGIA KURA GOLI BORA LA LIGI YA MABINGWA ULAYA...
Popular Posts
-
Mchezaji wa zamani wa klabu ya Real Madrid Ramon Calderon anafikiria kuwa klabu ya Manchester United itakuwa imetumia hekima kumsajili Ser...
-
ARSENAL INA MATUMAINI YA KUMNASA BENZEMA: Azma ya Arsenal kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema imepata mwamko mpya baada ...
-
KIIZA APEWA WIKI MBILI KUONGEZA KIWANGO
-
Chile imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Copa America baada ya kuichapa Uruguay 1-0, lakini mapema kipindi cha pili mshambuliaji...








0 comments:
Post a Comment