FALCAO KUBADILISHWA NA WACHEZAJI WATATU CHELSEA, GARAY KUTUA ARSENAL, LLORENTE AJIPELEKA LIVERPOOL...

Saturday, 27 June 2015

MONACO-Ruben Loftus-Cheek, Nathan Ake and Andreas Christensen:



Klabu ya Monaco imepanga kuwachukuwa kwa mkopo wachezaji watatu kutoka katika klabu ya Chelsea ikiwa kama ni moja ya mipango ya klabu hiyo kuwapatia kwa mkopo mshambuliaji Radamel Falcao. Wachezaji hao ni pamoja na Ruben Loftus-Cheek, Nathan Ake na Andreas Christensen.

ATLETICO MADRID-MARTINEZ:



Mchezaji wa kimataifa wa Colombia Jackson Martinez mwenye umri wa miaka 28 amethibitisha kuwa atajiunga na klabu ya Atletico Madrid kutoka klabu ya Porto kwa ada ya pauni milioni 24.8 na atapatiwa mkataba wa miaka minne.

LIVERPOOL-LLORENTE:



Baada ya Juventus kumpata mshambuliaji Mario Mandzukic kutoka Atletico Madrid, mshambuliaji aliyekuwa klabuni hapo Fernando Llorente anatazamiwa kujiunga na klabu ya Liverpool. Liverpool imekuwa ikimuhitaji mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30.

ARSENAL-EZEQUIEL GARAY:



Klabu ya Arsenal inaongoza mbio za kumuwania mlinzi wa kati wa klabu ya Zenit Ezequiel Garay. Klabu hiyo ya Uingereza imetoa ofa ya pauni milioni 13 ili kumnasa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. Klabu ya Manchester United ilihusishwa pia na mchezaji huyo.

TOTTENHAM-VICTOR MOSES:



Baada ya kuwa na kizungumkuti katika klabu ya Chelsea, Tottenham imepanga kufanya usajili wa kushitukiza wa mchezaji wa klabu hiyo Victor Moses. Mchezaji huyo amekuwa akihusishwa na kujiunga moja kwa moja na klabu ya Stoke City ambapo alikipiga kwa mkopo msimu uliokwisha, lakini huenda mpango huo akauchelewesha baada ya Spurs kuonesha nia.

0 comments:

Post a Comment