MANCHESTER UNITED - BASTIAN SCHWEINSTEIGER

Manchester United bado wana nia ya kumpata mchezaji wa Bayern Munich Bastian Schweinsteiger hata baada ya kumsaini Morgan Schneiderlin kutoka Southampton.
MANCHESTER CITY - PAUL POGBA

Manchester City wameanza mazungumzo na klabu ya Juventus kwa ajili ya kupata saini ya Paul Pogba. Txiki Begiristain amekutana na wakala wa kiungo huyo na kuambiwa mabingwa wa Italia wanahitaji £70.9m na Pogba anahitaji mshahara wa pound milioni £8.5 kwa mwaka.

Atletico Madrid wameungana na Olympique Marseille katika kinyang'anyiro cha kutafuta saini ya Karim Rekik kutoka Manchester City. beki huyo alikuwa kwa mkopo katika klabu ya PSV misimu miwili iliyopita.
ARSENAL - PETR CECH

Arsenal wamekubaliana na ofa ya euro milioni 15 kutoka Chelsea kwa ajili ya kumsaini Petr Cech. Dili hilo limepangwa kutangazwa siku ya Jumatatu.
STOKE CITY - STEVEN N'ZONZI

Stoke City wanampango wa kumpatia Steven N'Zonzi mkataba mpya ili kukwepa ofa toka kwa Sevilla na Leicester City.
MANCHESTER UNITED - SEAMUS COLEMAN

Manchester United wanajiandaa kuweka dau la £20m kwa ajili ya beki wa kulia wa Everton Seamus Coleman, kwa mjibu wa gateti la the Sun.
Antonio Valencia alicheza idadi kubwa ya mechi kama upande wa kulia msimu uliopita, lakini Louis van Gaal anahitaji kuleta mchezaji mtaalamu katika nafasi hiyo, na Coleman ni chaguo lake la kwanza.
MONACO - MATTIA DESTRO

Mshambuliaji wa Roma Mattia Destro aliyekuwa akiwaniwa na klabu ya Arsenal, lakini mchezaji huyo amekubali kujiunga na Monaco katika League 1 msimu huu kwa mjibu wa Sunday Express.
PSG - KEVIN TRAPP

Paris Saint-Germain wapo katika mazungumzo na klabu ya Bundesliga Eintracht Frankfurt juu ya ewezekano wa uhamisho wa golikipa Kevin Trapp. Mchezaji huyo mwenye miaka 24 amakili kufikia makubaliano binafsi na PSG.








0 comments:
Post a Comment