KLABU YA ARSENAL YASHITAKIWA KWA KUKIUKA MAADILI...

Friday, 12 June 2015



Klabu ya Arsenal imeshitakiwa kwa madai ya kukiuka maadili ya FA (Kanuni Za Wakala Wa Soka) kwa kufanya uhamisho wa mlinzi wa kulia wa klabu hiyo Calum Chambers kutoka Southampton .

Beki huyo aliwasili katika Uwanja wa Emirates majira yaliyopita kwa ada inayosadikika kuwa karibu Euro milioni 20.

Kauli rasmi ya FA inasomeka kwamba:
"Madai yanahusiana na uhamisho wa Calum Chambers kutoka Southampton kwenda Arsenal tarehe 26 Julai 2014.



"Wakala aliyeidhinisha uhamisho huo Alan Middleton pia ameshitakiwa kwa tuhuma za kukiuka maadili ya FA (Kanuni Za Wakala Wa Soka) kuhusiana na uhamisho huo.

"Mr Middleton amepewa muda hadi tarehe 17 Juni 2015 ili kukabiliana na shitaka hilo.

"Arsenal nayo imepewa muda hadi tarehe 26 Juni 2015 baada ya klabu hiyo kuomba muda zaidi wa kukabiliana na shitaka linalowakabili."

0 comments:

Post a Comment