MEMPHIS DEPAY ATUA RASMI OLD TRAFFORD....

Friday, 12 June 2015

Embedded image permalink

Manchester United imethibitisha usajili wa mchezaji Memphis Depay kutoka PSV kwa ada ya Euro milioni 30.8 uliokamilika mwanzoni mwa mwezi wa tano licha ya kuwepo kwa upinzani kutoka kwa klabu ya Liverpool iliyoonesha nia ya kumtaka mchezaji huyo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 alikubali kuhamia Old Trafford mapema mwezi wa tano kabla ya dili kuthibitishwa rasmi siku ya Ijumaa.


Tovuti ya Goal imetabanaisha kwamba msimu uliopita kocha wa klabu ya Manchester United Louis van Gaal alizungumza na Depay akimshauri kubaki PSV kwa mwaka mmoja zaidi kabla ya kuhamia Old Trafford, na baada ya kushinda kampeni za Eredivisie, hatimaye mshambuliaji huyo amesaini rasmi mkataba wa miaka minne na klabu ya Man Utd.

Embedded image permalink

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi alisema,"Kwangu mimi hii ni kama ndoto iliyokuwa kweli; kucheza katika klabu kubwa duniani na kupata nafasi ya kufanya kazi na mtu ambaye binafsi naamini ni kocha bora duniani Louis van Gaal.

"Nina imani kubwa sana na uwezo wangu na nitafanya kazi kwa bidii kuweza kukamilisha ndoto zangu.

"Nimekuwa na PSV Eindhoven tangu nikiwa na umri wa miaka 12 na ninapenda kuwashukuru kwa kila kitu. Ulikuwa ni wakati wa furaha sana pale tuliposhinda ligi na nilifurahi sana kuwa sehemu ya furaha hiyo. Huu sasa ni ukurasa mpya katika maisha yangu na niliokuwa nikiutegemea.

Louis van Gaal aliyemchukua Depay kwenye Mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2014 kama sehemu ya kikosi cha Uholanzi amesema: " Ninamfahamu Memphis vizuri tangu kipindi tunafanya kazi pamoja katika timu ya taifa ya Uholanzi. Ni kijana ambaye anaweza kucheza nafasi tofauti uwanjani.



"Itamchukuwa muda Memphis kuendana na ligi ya Uingereza lakini sina shaka ana vigezo vya kuwa mcheza mpira mashuhuri kwa klabu yake na yupo katika klabu inayofaa kuendeleza kazi nzuri ambayo amekwishaifanya."


0 comments:

Post a Comment