MAJINA YA WACHEZAJI NYOTA AMBAO ARSENAL IMESHINDWA KUWASAJILI KATIKA MISIMU TOFAUTI...

Monday, 22 June 2015



Mashabiki wa klabu ya Arsenal watakuwa wanaombea kwamba jina la Geoffrey Kondogbia lisiwe katika orodha ya majina ya wachezaji wakubwa klabu hiyo imeshindwa kuwasajili lakini itabaki kuwa "ingekuwa" baada ya kiungo huyo mkabaji wa klabu ya Monaco kukubali kujiunga na klabu ya Inter Milan siku ya Jumapili.

Pamoja na kocha wa Arsenal Arsene Wenger kumzungumzia mchezaji huyo kwa miaka kadhaa, mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa amesaini katika klabu ya Inter Milan kwa ada ya pauni milioni 25.

Arsenal imeshindwa kuwasajili baadhi ya wachezaji nyota licha ya kuwazungumzia mara kwa mara  katika vipindi tofauti tofauti vya usajili. Hawa ni baadhi ya wachezaji klabu hiyo ya Arsenal imeshindwa kuwaleta klabuni hapo katika misimu tofauti.

1. Lionel Messi
2. Cristiano Ronaldo
3. Gerard Pique
4. Zlatan Ibrahimovic
5. Yaya Toure
6. Gareth Bale
7. Geoffrey Kondogbia

0 comments:

Post a Comment