MAN CITY YATENGA £40 MILIONI KUMPATA WILSHERE, OTAMENDI ATOA TAMKO KUHUSU MAN UTD...

Saturday, 20 June 2015

MANCHESTER CITY-WILSHERE:



Manchester City inajiandaa kutoa dau la pauni milioni 40 ili kumpata kiungo wa klabu ya Arsenal Jack Wilshere kama watamkosa kiungo wa miamba ya Italia klabu ya Juventus Paul Pogba. Manchester City wapo tayari kumlipa kiungo huyo mshahara wa pauni 150,000 kwa wiki.

MANCHESTER UTD-OTAMENDI:



Mlinzi wa klabu ya Valencia Nicolas Otamendi amewaambia marafiki zake kuwa yupo tayari kujiunga na klabu ya Manchester Utd. Valencia imewataka Manchester United kulipa dau la pauni milioni 35 kumnasa mchezaji huyo.

CHELSEA-ALDERWEIRELD:



Meneja wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho anachelewesha mpango wa kubadilishana wachezaji kati ya Filipe Luis na Toby Alderweireld huku akiangalia namna nyingine ya kupata mlinzi mpya katika klabu hiyo.

PSG-GRIEZMANN:



PSG imetoa ofa yake ya euro milioni 40 kwa klabu ya Atletico Madrid kwa ajili ya kupata saini ya mchezaji Antoine Griezmann. Mabingwa hao wa Ufaransa wameachana na mawazo ya kumpata mchezaji wa Manchester United Angel Di Maria na mchezaji wa Juventus Paul Pogba.

0 comments:

Post a Comment