RAMOS AITAMANI BARCELONA, CECH KULIPWA MSHAHARA MNONO ARSENAL...

Friday, 19 June 2015

REAL MADRID-SERGIO RAMOS



Taarifa kutoka Hispania zinaeleza kuwa mazungumzo kati ya Real Madrid na beki wake wa kati Sergio Ramos yamevunjika, huku wakala wa mchezaji huyo akizungumza na mmoja wa wagombea uraisi wa klabu ya Barcelona Jordi Majo kuhusiana na mchezaji huyo kutua katika klabu hiyo.

MANCHESTER UTD-FIRMINO



Mchezaji wa Hoffenheim Roberto Firmino amekubali ofa kutoka Manchester United, hili ni pigo kwa klabu pinzani ya Liverpool ambayo ilikuwa ikimuwania mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazili. Nyota huyo atatua katika klabu ya Manchester United kwa dau la euro milioni 21.


ARSENAL-SVEN BENDER & SOKRATIS PAPASTATHOPOULOS



Arsene Wenger anafikiria kutoa ofa kwa wachezaji wawili wa klabu ya Borussia Dortmund Sven Bender na Sokratis Papastathopoulos. Bosi mpya wa Thomas Tuchel yupo tayari kuwauza wachezaji hao ili kusuka kikosi chake na klabu ya Arsenal ipo tayari kutoa ada ya euro milioni 42 kwa wachezaji hao.


LIVERPOOL-MATEO KOVACIC



Baada ya Steven Gerrard kuondoka, kocha wa Liverpool Brendan Rodgers ana nia ya kumleta kiungo mpya katika klabu hiyo na anamtaka nyota wa Inter Mateo Kovacic. Wekundu hao wako tayari kutoa dau la euro milioni 30.


ARSENAL-PETR CECH



Arsenal ipo tayari kumfanya Petr Cech kuwa golikipa anayelipwa pesa nyingi katika klabu hiyo na mmoja ya wachezaji watakao kuwa wanapokea mshahara zaidi ya £ 100,000 kwa wiki katika klabu hiyo. Mchazaji huyo wa kimataifa wa Czech anajianda kuondoka Chelsea, lakini Arsenal wanaweza kupata upinzani kutoka PSG ambayo inamuwania kipa huyo.


ARSENAL-ARTURO VIDAL



Manchester United na Real Madrid wamejitoa kwenye mbio za kumuwania kiungo wa Juventus Arturo Vidal baada ya kukamatwa akiendesha gari huku amelewa. Hii inaiachia njia klabu ya Arsenal kumsajili kiungo huyo.


BARCELONA-PAUL POGBA



Ripoti kutoka Barcelona zinadai kuwa klabu hiyo ipo tayari kuwauza baadhi ya wachezaji ili kujipatia kiasi cha pesa cha euro milioni 100 ili kumnunua kiungo wa klabu ya Juventus Paul Pogba.

0 comments:

Post a Comment