MANCHESTER CITY YAMRUDIA STERLING KWA KISHINDO...

Tuesday, 16 June 2015



Manchester City inajiandaa kutoa dau la pauni milioni 40 kwa klabu ya LIverpool ili kumpata mshambuliaji Raheem Sterling.

Tovuti ya Goal imetanabaisha kwamba Liverpool ilikataa dau la pauni milioni 25 pamoja na pauni milioni 5 kama nyongeza iliyotolewa na City wiki iliyopita.

Manchester City imepanga kurudi na dau kubwa la pauni milioni 35 pamoja na nyongeza ya pauni milioni 5 kwa jitihada za mchezaji huyo.

City imepanga kutumia pauni milioni 40 kupata saini ya Sterling, ambaye anaonekana kutaka kutimka klabuni hapo baada ya wakala wake Aidy Ward kuthibitisha kuwa mchezaji huyo hatoongeza mkataba na klabu hiyo ya Liverpool "The Reds".



Mkataba wake wa sasa na Liverpool aliosaini mwaka 2012, unamalizika mwaka 2017, na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 amekataa mkataba wa pauni 100,000 kwa wiki kubaki katika klabu hiyo.

Ikiwa pamoja na Sterling, tovuti ya Goal inaelewa kuwa klabu ya Manchester City inamuwania mchezaji nyota wa Hoffenheim Roberto Firmino.



Wakala wa Mbrazili huyo, Roger Wittmann, alithibitisha Jumatatu kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 atahamia Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu.

0 comments:

Post a Comment