ROBERTO FIRMINO KUCHEZA MANCHESTER UTD MSIMU UJAO...

Monday, 15 June 2015



Kiungo wa kimataifa wa Brazili na klabu ya Hoffenheim Roberto Firmino atajiunga na klabu mojawapo ya Ligi Kuu Uingereza, kwa mujibu wa wakala wake.

Imeripotiwa kuwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 ameivutia klabu ya Manchester United baada ya kufanya vizuri huko Bundesliga, amefunga magoli 49 katika mechi 153, na ushindi alioipatia Brazili dhidi ya Honduras kwenye mashindano ya Copa Amerika umempa nafasi kubwa ya kutua Ligi Kuu Uingereza.

Firmino alisaini mkataba mpya wa miaka mitatu katika klabu yake ya Hoffenheim mwaka 2014 , lakini Louis van Gaal anasadikika kuwa karibu kukubaliana na mpango wa kumsajili kwa ada ya pauni milioni 13.

"Ninachoweza kusema ni kwamba atakwenda Uingereza, " Roger Wittmann alinukuliwa akizungumza na Bild.

Liverpool pia wamekuwa wakihusishwa kuwania saini ya Firmino baada ya Raheem Sterling kusema ataondoka Anfield kutafuta malisho mapya.



Hivi karibuni Firmino aliingia kama mchezaji wa akiba akitokea benchi kama mbadala wa Fred katika mechi dhidi ya Peru ambapo Brazil iliibuka na ushindi wa goli 2-1 kwenye mashindano ya Copa Amerika Jumapili jioni.

0 comments:

Post a Comment