"MARTINEZ ATANG'AA AKITUA ARSENAL"-THIERRY HENRY

Tuesday, 16 June 2015



Thierry Henry anahisi Jackson Martinez atang'aa katika klabu ya Arsenal huku kukiwa na uvumi kuwa mchezaji huyo atatua katika uwanja wa Emirates.

Wiki iliyopita iliaminika kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 yupo mbioni kujiunga na klabu ya AC Milan kutoka Porto, ingawa mchezaji huyo amekanusha habari hizo.

Mwezi wa pili meneja wa Arsenal Arsene Wenger alizungumzia kuhusu mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Colombia, akisisitiza mshambuliaji "yupo katika orodha ya vilabu vingi," na shujaa wa klabu hiyo Henry amemsifia Martinez kufuatia uamuzi wake unaotarajiwa.

"Jackson Martinez anaweza kufiti vizuri." Henry aliwaambia waandishi wa habari. "Lakini tayari unaye Giroud ambaye kiasi wanafanana kama mshambuliaji."



"Anaweza kuwa nyongeza nzuri katika kikosi. Alikuwa na msimu mzuri katika Ligi ya Mabingwa, lakini tayari una watu."

"Nadhani Giroud ni zaidi au chini ya mchezaji wa aina hiyo. Nadhani Martinez ana nguvu kiasi na anaweza kurudi nyuma kusaidia lakini tutaona ni nini Arsene Wenger atafanya."

"Kwa ujumla, washambuliaji wa Arsenal hawakufanya vibaya msimu uliokwisha."

0 comments:

Post a Comment