MESSI AIKATAA TUZO YA MCHEZAJI WA MECHI...

Tuesday, 16 June 2015



Nahodha wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi alikataa tuzo ya mchezaji wa mechi baada ya timu yake kutoa sare ya 2-2 dhidi ya timu ya taifa ya Paraguay, kwasababu alikuwa na hasira baada ya kupoteza pointi mbili katika mechi hiyo ya ufunguzi ya mashindano ya Copa Amerika.

Messi ambaye aliisaidia timu yake kupata goli la pili kupitia mkwaju wa penati baada ya Kun Aguero kuipatia timu hiyo bao la kuongoza hakuwa na hamu ya picha baada ya filimbi ya mwisho kupulizwa siku ya Jumamosi.

Mwakilishi kutoka MasterCard, ambaye huwa anatoa tuzo hizo kwenye mashindano ya bara, alikwenda kwenye chumba cha Argentina cha kubadilishia nguo kumjulisha mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kuwa amechaguliwa kama mchezaji wa mechi lakini aliambiwa kuwa Messi hawezi kupokea tuzo hiyo.

Kufuatia kukataa kwa mshambuliaji huyo wa Barcelona, MasterCard walikuwa na nia ya kumchagua mchezaji mwingine kutoka kwenye kikosi cha vijana hao wa Gerardo Martino lakini hakuna mchezaji aliyekuwa tayari kupokea tuzo hiyo.

Baadae tuzo hiyo ilipendekezwa itolewe kwa mmoja wa wachezaji waliofunga mabao kutoka timu pinzani, kati ya Nelson Valdez ambaye aliipatia timu yake goli la kuongoza au Lucas Barrios ambaye aliipatia timu yake bao la kusawazisha.

Leo katika mchezo wa kundi B Argentina watamenyana vikali na timu ya Uruguay.

0 comments:

Post a Comment