MESSI VS RONALDO

Friday, 12 June 2015

Mshambuliaji hatari wa Barcelona Lionel Messi amesisitiza kuwa "hakuna ushindani" kati yake na nyota wa Real Madrid Christiano Ronaldo.

Wakali hao wawili ndio wanaodhaniwa kuwa wachezaji wa kiwango cha juu kuwahi tokea duniani huku wakishinda kwa nyakati tofauti ndani ya miaka saba iliyopita tuzo za ulaya zijulikanazo kama Ballons d'Or.

Makali ya Mreno huyo ndani ya miaka miwili iliyopita yamemfanya kuwa mchezaji bora wa ulaya mara mbili hivyo kumuongezea chachu ya kufanya vizuri zaidi lionel messi msimu huu sanjali na kuiongoza klabu yake ya barcelona kutwaa mataji matatu msimu huu na kudhaniwa kua mwanasoka wa kwanza muagentina kufikia mafanikio hayo.

kadhalika MESSI ameendelea kutanabaisha kuwa haathiliwi na chochote kile afanyacho ndani na nje ya uwanja RONALDO. 

0 comments:

Post a Comment