MGOGORO WA SIMBA NA SINGANO WAFIKA SERIKALINI...

Saturday, 13 June 2015

Wiki iliyopita sakata hilo lilitolewa ufafanuzi na Shirikisho la soka Tanzania TFF, lakini baada ya kikao hicho mambo yalibadilika kwa pande zote mbili kupingana na maamuzi
HATIMAYE mgogoro kati ya winga Ramadhani Singano ‘Messi’ na klabu yake ya Simba kuhusiana na kuisha kwa mkataba umefika Serikalini.

Wiki iliyopita sakata hilo lilitolewa ufafanuzi na Shirikisho la soka Tanzania TFF, lakini baada ya kikao hicho mambo yalibadilika kwa pande zote mbili kupingana na maamuzi hasa mchezaji akidai yeye ni sawa na mchezaji huru na jana ameonekana kwenye ofisi za klabu ya Azam ambayo inatajwa kumuwania.
Kauli ya serikali kupitia kwa Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Juma Nkamia, amezitaka pande hizo kuacha malumbano badala yake kufuata kile walichoelekezwa na TFF.

Nkamia ameiambia Goal hawapendi kuona swala hilo likizidi kupasua vichwa vya wapenda michezo nchini hivyo nivyema waka fuata kile kilichoamuliwa na TFF na ikishindikana basi Shirikisho linapaswa kutoa maamuzi mengine yatakayo kuwa na hekima na kutouumiza upande wowote.

Singano amewahi kukaririwa na Mtandao huu wa Goal kwamba hatoweza kufikia makubaliano ya kuichezea tena klabu hiyo na hivyo yeye ni mchezaji huru anayesaka timu ya kuchezea msimu ujao.

Azam inapewa nafasi kubwa ya kumtumia mchezaji huyo aliyeanza kuichezea Simba tangu akiwa na umri w miaka 16 akiwa timu ya vijana kabla ya kupandishwa misimu mitatu iliyopita.

0 comments:

Post a Comment