TAIFA STARS YAWASILI MISRI...

Saturday, 13 June 2015

TIMU ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imewasili salama katika eneo la Borg El Arab jijini Alexandria tayari kwa mchezo wake wa kesho dhidi ya wenyeji wao Misri
TIMU ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imewasili salama katika eneo la Borg El Arab jijini Alexandria tayari kwa mchezo wake wa kesho dhidi ya wenyeji wao Misri ukiwa ni mchezo wa kundi G kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika AFCON.

Kocha mkuu wa Stars Mart Nooij, atakiongoza kikosi chake katika mazoezi ya mwisho leo saa 1 usiku katika uwanja wa Borg El Arab kwa saa za Misri, sawa na saa 2 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Msemaji wa Shirikisho la soka Tanzania TFF, Baraka Kizuguto ameaimbia Goal kutoka Misri wachezaji wote wa timu hiyo wapo katika hali nzuri na wamepania kupata ushindi katika mchezo huo wa ugenini.
Kizuguto amesema mchezo wa kesho ni muhimu kwa Stars kupata ushindi ili kurudisha imani ya Watanzania ambao wamekosa raha kutokana na matokeo ya timu hiyo katika siku za karibuni.

Naye kiungo Amri Kiemba ameungana na wachezaji wengine waliokuwa kambini Addis Ababa kuchukua nafasi ya Mrisho Ngasa ambaye alishindwa kuungana na timu kutokana na sababu zilizopo nje ya uwezo wake.
Mchezo kati ya Misri na Tanzania utachezwa kesho saa 2 usiku kwa saa za Afrika Mashariki na kati katika uwanja wa jeshi la Misri (Borg El Arab) uliopo takribani kilometa 70 kutoka jijini Alexandria na kilometa 200 kutoka jiji la Cairo.

0 comments:

Post a Comment