MKURUGENZI WA MAWASILIANO NA MAMBO YA UMMA WA FIFA AACHIA NGAZI

Thursday, 11 June 2015



Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mambo ya umma wa Shirikisho La Mpira Duniani (FIFA) ameamua kuachia ngazi hiyo.


Walter De Gregorio alifanya kazi katika chombo cha kusimamia michezo tangu Septemba 14, mwaka 2011 na ataendelea kuwa mshauri wa Shirikisho hilo hadi mwishoni mwa mwaka huu.

Hata hivyo, naibu wake, Nicolas Maingot, amekaimu nafasi hiyo kwa muda.

"Walter amefanya kazi kwa bidii na kwa kujitoa kwa miaka minne na tunashukuru kwa dhati kwa yote aliyoyafanya," Katibu Mkuu Jerome Valcke aliiambia rasmi tovuti ya shirika hilo.

"Nafurahi bado tutaendelea kufanya kazi chini ya utaalamu wake hadi mwishoni mwa mwaka huu"

Uswisi-Italia inasadikiwa kuwa moja kati ya msaada mkubwa kwa Raisi wa Shirikisho la Mpira Duniani (FIFA) Sepp Blatter, ambaye wiki iliyopita alitangaza kujiuzulu kutokana na kuibuka kwa sakata la rushwa ambalo limekumba shirikisho hilo.

De Gregorio alisimamia mikutano ya wanahabari ambayo ilihusisha kujiuzulu kwa Raisi wa Shirikisho hilo Sepp Blatter pamoja na kutoa uthibitisho kwamba kuna maofisa wa FIFA walikamatwa, zoezi lililoendeshwa na Shirika la KIjasusi la Marekani (FBI) kuhusiana na shutuma za hongo tangu mwaka 1991.

0 comments:

Post a Comment